BUKOBA SPORTS

Tuesday, July 17, 2012

FABIO CAPELLO ATANGAZWA KUWA KOCHA WA URUSI

Fabio Capello
Fabio Capello leo ametangazwa kama kocha mpya wa timu ya Taifa ya Urusi na anatarajiwa kukamilisha mambo mengine ya mkataba wake siku zijazo.
Kocha huyo wa zamani wa Uingereza, alikuwa na maongezi na chama cha mpira cha Urusi, Russian Football Union (RFU) wiki iliyopita kwa ajili ya kuweza kumfanya awe kocha wao.
Warusi wamesema ya kuwa wanaamini Fabio ndio mtu sahihi wa kuisaidia timu hiyo kuweza kurudi katika kiwango chake tena baada ya kuboronga katika mashindano ya Euro 2012.
“Tunatangaza leo ya kuwa tumeamua kumpa kazi ya ukocha wa timu ya taifa wa Urusi Fabio Capello” alisema Nikita Simonyan ambaye ni Makamu wa raisi wa RFU.

No comments:

Post a Comment