Manchester City wanamfuatilia kwa karibu mchezaji wa Celtic anayetokea Kenya Victor Wanyama.
Mabingwa hao wa ligi ya Uingereza wanawasiwasi na mchezaji wao Gareth Barry ambaye ni majeruhi. Na kuna uwezekano mkubwa akawa hayupo fiti pindi msimu mpya utakapo anza.
Nafasi hiyo ya kiungo mkabaji inachezwa na Barry au De Jong. Barry ndio huyo anaumwa na De Jong inasemekana yupo mboni kuondoka klabuni hapo.
Wanyama mwenye umri wa miaka 21,ambaye ameonesha nia ya kuihama klabu yake ya Celtic anafuatiliwa kwa karibu na klabu nyingi za Uingereza zikiwemo Liverpool, Newcastle na QPR.
Chanzo: Mpiratz
No comments:
Post a Comment