
Akizungumza nami mtaarishaji na muanzilishi wa kipindi hicho Masud Kipanya amesema kuwa watu wengi walidhani maisha Plus imekufa lakini ilisimama kwa vile ilibidi mabadiliko makubwa yafanyike ili kuboresha “maisha Plus haikufa wala kuondoka isipokuwa tulisimamamisha mwaka jana ili tufanye maboresho ikiwa ni pamoja na kufunga Camera na mic za kisasa pale kijijini na kuboresha miundo mbinu zaidi” alisema Masoud.
Audition itaanza mwezi ujao na itaanzia Arusha na kuzunguka mikoa tofauti na hatimaye mwezi wa kumi washiriki wataingia kijijini rasmi. Aidha Masoud aliongeza kuwa umri ni kati ya miaka 21 na 26 huku akisema kigezo cha elimu ni kidato cha nne “age 21-26, elimu O’level, na ujue jinsi ya kuishi, Ukiwa na ujuzi wa ziada ni faida zaidi” alisema Kipanya. Aidha Masoud ameongeza kuwa kipindi cha Maisha Plus kitarushwa na Television ya TBC ambapo kila kitu kimekamilika na atawajulisha mashabiki muda na wakati ambapo kipindi hiki kitakuwa hewani.
Kipindi cha Maisha Plus kimejizolea umaarufu mkubwa kutokana na kuwa na mguso wa maisha halisi na tamaduni sio tu za Kitanzania bali za kiafrika zaidi.
SOURCE:http://spotistarehe.wordpress.com
No comments:
Post a Comment