BUKOBA SPORTS

Sunday, July 22, 2012

STORY FUPI YA KIFO CHA MTOTO WA USHER


Kyle Glover
Hatimaye mtoto wa kufikia wa Usher,Kyle Glover amefariki dunia wiki mbili baada ya kujeruhiwa katika ajali ya boti.
Mtoto huyo wa mke wa zamani wa Usher,Tameka Foster amefariki jana asubuhi kwenye hospitali aliyokuwa amelazwa mjini Atlanta.
Kyle aligongwa na boti kichwani wakati akicheza kwenye ziwa Lanier.
Kwa muda wote huyo mtoto huyo alikuwa amewekewa mashine maalumu ya kumsaidia kuishi.

Kabla ya ajali hiyo Usher,ambaye jina lake halisi ni Usher Raymond, alikuwa kwenye vita kali na mke wake huyo wa zamani ya kugombania watoto.

No comments:

Post a Comment