BUKOBA SPORTS

Sunday, July 22, 2012

CHELSEA WAFANYA MAZOEZI UWANJANI BAADA YA NDEGE KUCHELEWA!!!

Mara nyingi ndege ikichelewa watu huwa wanalala, wanasoma vitabu au wanafanya booking nyingine na kuondoka uwanjani ila kwa Chelsea sijui ndo Ubingwa wa Ulaya unawachanganya mpaka wakaamua kuanza fanya mazoezi hapo hapo uwanjani.
haya kama ndege
Chelsea wanasafiri kuelekea New York amabako watacheza mechi ya kirafiki na PSG katika uwanja wa Yankee.
Di Matteo anataka timu yake isahau swala la kuwa wao ni mabingwa wa Ulaya  na waanze kufikiria kuwa mabingwa wa Uingereza pindi mwezi wa nane utakapofika.
Di matteo aliongea na waandishi wa habari tangia alipochaguliwa kuwa kocha rasmi wa Chelsea.
“Wiki zile 12 zilikuwa wiki za maajabu sana kwangu, tulikuwa twagombania nafasi ya nne, FA cup na Champions League.Ilikuwa
inatubidi tujipange kwelikweli”. Alisema Di Matteo
Chelsea wanafanya kama walivyofanya mwaka 2004 kusajili wachezaji wengi kadri wawezavyo ili kuweza imarisha kikosi chao.
KWA HISANI YA MPIRA TZ

No comments:

Post a Comment