BUKOBA SPORTS

Wednesday, July 18, 2012

MECHI YA KIRAFIKI YA MACHESTER UNITED V AMA ZULU KUCHEZWA LEO USIKU SAA 19:00 BST, SHINJI KAGAWA KUCHEZA


Shinji Kagawa amesema kuwa anaanza kuyazoea vizuri maisha ya England baada ya kuihama Borussia Dortmund ya Ujerumani na kutua Manchester United.
Kagawa, Mchezaji wa Kimataifa wa Japan ambaye amejiunga na Man United kwa dau la Euro Milioni 22, anatarajiwa kucheza Mechi yake ya kwanza leo Usiku huko Durban, Afrika Kusini dhidi ya Ama Zulu ikiwa ni Mechi ya Kirafiki ambayo pia ni ya kusheherekea Mandela Dei.
Akiandika kwenye Blogu yake, Kagawa amesema: ‘Mji wa Manchester ni tofauti na Dortmund. Bado najiona kama Mtalii, kila kitu kipya na kinafurahisha. Manchester imetulia na muda hupita pole pole. Nadhani ina mazingira mazuri kwa Mwanasoka.’
Akiwa na Man United, Kagawa atavaa Jezi Namba 26 ambayo ni Namba aliyokuwa akiivaa huko Cerezo Osaka, Klabu yake ya Japan kabla hajahamia Borussia Dortmund.
Pia, Kagawa ametoa shukrani zake kwa Borussia Dortmund na Mashabiki wake kwa kumwezesha kupanda chati na kutua Man United.
Akithibitisha kuwa Kagawa atacheza Mechi dhidi ya Ama Zulu, Meneja wa Man United, Sir Alex Ferguson, alisema: ‘Kipau mbele ni kuwafanya Wachezaji wetu wenye uzoefu wawe fiti lakini Wachezaji Vijana watacheza kila Mechi. Upo uwezekano Kagawa na Chicharito wakaanza pamoja.’
Hata hivyo kuna uwezekano baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza cha timu hiyo wakashindwa kwenda Bondeni akiwamo Wayne Rooney.

Ikiwa uko, itacheza dhidi ya timu ya AmaZulu na Ajax Cape Town.
Rooney, Phil Jones, Ashley Young, Danny Welbeck (England), Patrice Evra (Ufaransa) na Nani (Ureno) wako likizo baada ya kuchelewa kwenda mapumzikoni kutokana na kushiriki kwao michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya mwaka huu.
Mkongwe Ryan Giggs, Tom Cleverly na David De Gea nao hawatakuwapo kwa sababu ya maandalizi ya michuano ya Olimpiki baadaye mwezi huu.
Pia kuna majeruhi kadhaa kama Nemanja Vidic, Chris Smalling na Darren Fletcher.
Hiyo ima maana, Kocha Alex Ferguson atakuwa na wachezaji wachache wenye majina kwenye ziara hiyo kama Ferdinand, Paul Scholes na Javier 'Chicharito' Hernandez.

PROBABLE LINEUP
AMAZULU FC

Amazulu
KapiniTeysie, Van Heerden, Nyadombo, Bukasa
Zhuwawo, Johnson, Mbhele, SenameleA. Dlamini, G. Dlamini
MANCHESTER UNITED

LindegaardVermijl, Ferdinand, Wootton, Brady
Carrick, Scholes
Valencia, Kagawa, Powell
Hernandez
 HISANI YA MTANDAO WA SOKA IN BONGO

No comments:

Post a Comment