BUKOBA SPORTS

Monday, July 23, 2012

MENEZES AWAEPUSHA VIJANA WAKE NA VISHAWISHI KWA KUWAFICHA HOTELINI JIJINI LONDON.

KOCHA wa kikosi cha timu ya taifa ya Brazil ambacho kitashiriki michuano ya Olimpiki Mano Menezes amesema kuwa wamechagua sehemu tulivu mbali na kijiji cha wanamichezo watakaoshiriki michuano hiyo ili kuepuka vishawishi. Kikosi cha timu hiyo kiko katika shinikizo kubwa la kurejea nyumbani wakiwa na medali ya dhahabu ya kwanza kwa nchi hiyo kwenye michuano hiyo na Menezes anaamini kuwa wana nafasi nzuri zaidi ya kufanya hivyo wakiwa katika hoteli waliyofikia iliyopo Hertfordshire nje kidogo ya jiji la London. Menezes amesema hayo wakati kikosi hicho kilipotembelea hifadhi hiyo maalumu kwa ajili ya michuano ya olimpiki kwa ajili ya kufanya manunuzi katika maduka makubwa yaliyopo katika maeneo ya kijiji hicho. Kikosi hicho cha wachezaji chini ya umri wa miaka 23 kinaongozwa na mshambuliaji nyota Neymar mwenye umri wa miaka 20, na kwasasa kikosi hicho kinafanya mazoezi mazoezi katika uwanja unaotumiwa na timu Arsenal uliopo kaskazini mwa jiji la London. Brazil itacheza na timu za Misri, Belarus na New Zealand katika michezo ya makundi na kikosi hicho ambacho kinategemewa kuwa ndio kikosi kamili cha nchi hiyo katika michuano ya Kombe la Dunia itakayochezwa miaka miwili ijayo nchini Brazil, kinapewa nafasi kubwa na kuondoka na medali ya dhahabu.
www.beki3.blogspot.com

No comments:

Post a Comment