BUKOBA SPORTS

Saturday, September 29, 2012

ENGLISH PREMIER LEAGUE: CHELSEA USO KWA USO NA ARSENAL, UNITED VS SPURS

KLABU ya Chelsea inatarajia kuendelea kujikita kileleni mwa Ligi Kuu nchini Uingereza kwa kushinda mchezo wao wa kesho dhidi ya mahasimu wao wa jiji la London Arsenal katika mchezo wao wa kwanza toka nahodha wao John Terry afungiwe kutokana na ubaguzi wa rangi.
Terry amefungiwa mechi nne na Chama cha Soka cha Uingereza-FA jana baada ya kukutwa na hatia ya kumfanyia vitendo vya ubaguzi wa rangi beki wa timu ya Queens Park Rangers-QPR Anton Ferdinand na pia kutozwa faini ya paundi 220,000. Terry amepewa siku14 toka atapopokea barua ya uamuzi uliofikiwa na FA kukata rufani kama hakuridhishwa na hukumu hiyo aliyopewa kufuatia tukio hilo ambalo lilitokea wakati wa mchezo wa baina ya Chelsea na QPR uliochezwa katika Uwanja wa Loftus Road Octoba 23 mwaka jana.  Adhabu hiyo haitaanza kufanya kazi mpaka muda wa kukata rufani utakapokwisha hiyo inamaanisha kuwa beki huyo atakuwepo katika mchezo wa leo dhidi ya Arsenal ambao utachezwa katika Uwanja wa Emirates. Jumamosi Septemba 29 zipo Mechi 8 za Ligi Kuu England [Barclays Premier League, BPL] na kati ya hizo zile zenye mvuto mkubwa, BIGI MECHI, ni ile itayofungua Dimba la Wikiendi itakayochezwa Uwanja wa Emirates kati ya Arsenal na Chelsea na ile itayofunga dimba Siku hiyo hiyo huko Old Trafford kati ya Manchester United na Tottenham Hotspur.

BPL: RATIBA MECHI ZA WIKI HII
Jumamosi Septemba 29
[Saa 8 Dak 45 Mchana]
Arsenal v Chelsea
[Saa 11 Jioni]

Everton v Southampton
Fulham v Manchester City
Norwich City v Liverpool
Reading v Newcastle United
Stoke City v Swansea City
Sunderland v Wigan Athletic
[Saa 1 na Nusu Usiku]
Manchester United v Tottenham Hotspur
Jumapili Septemba 30
[Saa 12 Jioni]
Aston Villa v West Bromwich Albion
Jumatatu Oktoba 1
[Saa 4 Usiku]
Queens Park Rangers v West Ham United

No comments:

Post a Comment