PAMOJA NA WENGER KUMTAKA THEO WALCOTT KUWA MPOLE,BAYERN MUNICH WAMTOLEA MACHO ILI AMRITHI FRANCK RIBERY
Bayern Munich
wanafuatilia mchakato wa kusainiwa kwa mkataba mpya wa winga wa
Arsenal, Theo Walcott kwa nia ya kumnyakua ikibidi ili akarithi nafasi
ya winga wao Franck Ribery anayefukuziwa na klabu ya nchini kwao
Ufaransa ya matajiri wa PSG.
Walcott atakuwa huru kusaini
mkataba wa makubaliano ya awali na klabu nyingine kufikia Januari 1 na
kocha Arsene Wenger amekiri kwamba wanaweza kumuuza kama atakataa
kusaini mkataba mpya waliompa kabla ya krismasi.
Gazeti la TZ limesema kuwa Bayern wanafuatilia kwa karibu maendeleo ya kusainiwa kwa mkataba mpya wa Walcott.
No comments:
Post a Comment