BUKOBA SPORTS

Sunday, September 30, 2012

URUSI YATANGAZA MIJI ITAKAYOTUMIKA KOMBE LA DUNIA.

NCHI ya Urusi imetangaza miji 11 ambayo itakuwa wenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia 2018 ikiwa ni mradi wa kwanza mkubwa kufanywa na nchi toka kuanguka kwa iliyokuwa USSR. Michuano hiyo mikubwa kabisa duniani itachezwa katika miji ya Moscow, Saint Petersburg, Sochi mji ambao pia uwakuwa mwenyeji wa michuano ya Olimpiki ya kipindi cha baridi 2014, Kazan, Yekaterinburg, Kaliningrad, Nizhny Novgorod, Samara, Rostov-on-Don, Saransk na Volgograd. Katika sherehe hizo zilizokuwa zikionyeshwa moja kwa moja katika luninga, huku zikiongozwa na Rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Sepp Blatter na Waziri wa Michezo wa nchi hiyo Vitaly Mutkoongozwa miji miwili ya Yaroslavl na Krasnodar iliondolewa katika orodha iliyokuwa na miji 13. Tofauti na michuano ya Olimpiki ya kipindi cha baridi, Kombe la Dunia litaihitaji serikali kutumia mabilioni ya dola kwa ajili kuendeleza viwanja, utalii na miundo mbinu ya usafiri kwa nchi nzima. Urusi ilipewa nafasi ya kuandaa Kombe la Dunia 2018 katika uchaguzi uliogubikwa na utata Desemba mwaka 2010 ambapo ulishuhudia nchi ya Qatar nayo ikipewa nafasi ya kuandaa michuano 2022 kwa kuishinda Uingereza ambayo nayo ilikuwa inataka nafasi hiyo.

 

 

RONALDO ATAMANI KUWA MCHEZAJI ANAYELIPWA ZAIDI DUNIANI.
TAMAA ya mshambuliaji nyota wa klabu ya Real Madrid ya Hispania, Cristiano Ronaldo kuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani kunaongeza kukua kwa mgawanyiko ndani ya klabu hiyo kitendo ambacho kinavistua vilabu vingine tajiri barani Ulaya. Mmiliki wa klabu ya Chelsea pamoja na tajiri wa kiarabu anayemiliki Manchester City na klabu ya Paris saint-Germain ya Ufaransa ndio wanaoongoza katika orodha ya timu ambazo zinawinda saini ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 27. Mshahara wa Ronaldo wa Euro milioni 7.98 ambao ni nusu na mshahara anaopata Samuel Eto’o katika klabu ya Anzi ya Urusi unamfanya nyota huyo kuwa wa 10 miongoni mwa orodha ya wachezaji wanaolipwa zaidi duniani. Nyota alikuwa akihitaji nyongeza ya asilimia 50 katika mshahara wake lakini suala hilo litakuwa gumu katika klabu hiyo kutokana na hali mtikisiko wa kiuchumi ulioikumba nchi hiyo katika kipindi cha hivi karibuni. Mapema mwezi huu Ronaldo alihojiwa na kudai kuwa suala la kitaaluma ndilo linalomsababisha akose furaha na klabu hiyo inajua hilo kauli ambayo ilizua mijadala katika vyombo mbalimbali vya habari duniani juu ya mstakabali wa mbeleni wa nyota huyo.

KUHUSU CRISTIANO RONALDO

Cristiano Ronaldo dos Santos Aveiro, OIH, commonly known as Cristiano Ronaldo, is a Portuguese footballer who plays as a forward for Spanish La Liga club Real Madrid and is the captain of the Portuguese national team. 
Born: February 5, 1985 (age 27), Funchal
Weight: 84.5 kg
Height: 1.87 m
Salary: Euro 12,000,000 (2012)
Net worth: US$ 160 million (2012) therichest.org
Children: Cristiano Ronaldo Jr.


NILIPANGA KUMPUMZISHA TERRY - DI MATTEO.
MENEJA wa klabu ya Chelsea, Roberto di Matteo amekiri kuwa alitaka kumuondoa John Terry katika kikosi chake ambacho kiliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Arsenal katika Uwanja wa Emirates jana. Terry alijumuishwa katika kikosi hicho ikiwa ni siku mbili toka alipofungiwa mechi nne na kutozwa faini ya paundi 220,000 na Chama cha Soka nchini Uingereza-FA baada ya kukutwa na hatia ya kumfanyia ubaguzi wa rangi beki wa Queens Park Rangers, Anton Ferdinand. Adhabu imekuja kufuatia tukio baina ya timu hizo ambazo ni mahasimu wa Magharibi mwa jiji la London Octoba mwaka jana ingawa hatahivyo adhabu itaanza pale ambapo muda wa kukata rufani utakapokwisha. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Di Matteo ambaye ni kiungo wa zamani wa kimataifa wa Italia na Chelsea amesema kuwa alifikiri kumuacha nahodha wake huyo katika mchezo huo lakini uamuzi wa kumjumuisha ulikuwa mzuri kutoka kiwango bora alichoonyesha.

No comments:

Post a Comment