BUKOBA SPORTS

Sunday, September 30, 2012

ARSENAL 1 CHELSEA 2

UWANJANI EMIRATES, Chelsea leo imeshusha kipigo cha kwanza Msimu huu kwa Arsenal kwenye Ligi Kuu England baada ya kuwachapa Bao 2-1 na wao kuendelea kukaa juu kwenye Msimamo wa Ligi wakiwa na Pointi 16 kwa Mechi 6 huku bao zote za Chelsea zikifungwa kilaini kutoka frikiki.
Chelsea ndio walitangulia kufunga katika Dakika ya 20 kufuatia frikiki ya Juan Mata kuangunishwa vyema na Fernando Torres aliemkuta mkabaji wake Laurent Koscielny akiwa amezubaa.
Arsenal walisawazisha kwa bao tamu la Gervinho kwenye Dakika ya 42 baada ya kupokea pasi ndani ya boksi na kuzunguka na kuachia kigongo kilichotinga nyavuni juu.
Lakini Chelsea walipata ushindi katika Dakika ya 52 baada ya frikiki ya Juan Mata kumpita kila mtu na kumparaza Laurent Koscielny na kutinga wavuni.
Arsenal walicharuka kujiokoa toka kipigo lakini jitihada zao kupitia Lukas Podolski na Olivier Giroud, alieingizwa Kipindi cha Pili, ziliokolewa na Kipa Petr Cech.
VIKOSI:
Arsenal: Mannone; Jenkinson, Koscielny, Vermaelen, Gibbs; Arteta, Diaby; Ramsey, Cazorla, Podolski; Gervinho
Akiba: Mertesacker, Santos, Giroud, Walcott, Oxlade-Chamberlain, Djourou, Martinez.
Chelsea: Cech; Ivanovic, Luiz, Terry, Cole; Ramires, Mikel; Mata, Oscar, Hazard; Torres
Akiba: Turnbull, Romeu, Lampard, Moses, Cahill, Azpilicueta, Bertrand.
Refa: Martin Atkinson.

RATIBA/MATOKEO
Jumamosi Septemba 29
Arsenal 1 Chelsea 2
[Saa 11 Jioni]
Everton v Southampton
Fulham 1 v 2Manchester City
Norwich City v Liverpool
Reading v Newcastle United
Stoke City v Swansea City
Sunderland v Wigan Athletic
[Saa 1 na Nusu Usiku]
Manchester United v Tottenham Hotspur
Jumapili Septemba 30
[Saa 12 Jioni]
Aston Villa v West Bromwich Albion
Jumatatu Oktoba 1
[Saa 4 Usiku]
Queens Park Rangers v West Ham United

No comments:

Post a Comment