BUKOBA SPORTS

Sunday, September 30, 2012

BACLAYS PREMIER REAGUE: MANCHESTER UNITED 2 SPURS 3, KWA MARA YA KWANZA TANGU 1989!

Kwa mara ya kwanza tangu 1989, Tottenham wamefanikiwa kuifunga Manchester United bao 3-2 katika Mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa Old Trafford.
Spurs walitangulia kupata bao mbili kwa kuisambaratisha Difensi ya Man United kwa kutumia kasi iliyoonyesha uzito wa Difensi hiyo kwa bao za Fulbeki Jan Vertonghen na ‘mkimbiaji’ Gareth Bale.
Bao hizo 2-0 zilidumu hadi mapumziko.

Andre Villas-Boas akishangilia kwa nguvu kuona timu yake inashinda jana usiku.

Kipindi cha Pili Man United walibadilika na kuonyesha wazi wazi hawakustahili kufungwa Mechi hii pale alipoingizwa Wayne Rooney na kumtengenezea Nani kufunga bao la kwanza lakini hapo hapo Spurs, wakidhirisha udhaifu wa Difensi ya Man United, wakapiga bao la tatu kupitia Clint Dempsey.
Shinji Kagawa aliifungia Man United bao la pili na waliendelea kutawala lakini walishindwa kupata bao la kusawazisha licha ya kosa kosa nyingi.

Nani akifunga goli kupitia kiki lililopigwa kutokea kulia

Shinji Kagawa akipita kwenye msitu wa Spurs!
VIKOSI
Manchester United: Lindegaard; Rafael, Ferdinand, Evans, Evra; Carrick, Scholes; Nani, Kagawa, Giggs; Van Persie.
Akiba: De Gea, Wootton, Anderson, Cleverley, Hernandez, Rooney, Welbeck.
Tottenham Hotspur: Friedel; Walker, Gallas, Caulker, Vertonghen; Sandro, Dembele; Lennon, Dempsey, Bale; Defoe.

RATIBA
Jumapili Septemba 30
[Saa 12 Jioni]
Aston Villa v West Bromwich Albion
Jumatatu Oktoba 1
[Saa 4 Usiku]
Queens Park Rangers v West Ham United 
Jumamosi Oktoba 6
[Saa 8 Dak 45 Mchana]
Manchester City v Sunderland
[Saa 11 Jioni]
Chelsea v Norwich City
Liverpool v Stoke City
Swansea City v Reading
West Bromwich Albion v Queens Park Rangers
Wigan Athletic v Everton
[Saa 1 na Nusu Usiku]
West Ham United v Arsenal
Jumapili Oktoba 7
[Saa 9 na Nusu Mchana]
Southampton v Fulham
[Saa 11 Jioni]
Tottenham Hotspur v Aston Villa
[Saa 12 Jioni]
Newcastle United v Manchester United
_____________________________________________________________
MATOKEO YOTE YA MECHI ZA JANA
Sunderland        1 Steven Fletcher 51                                  
Wigan Athletic    0                                                     
Kadi nyekundu: Jordi Gomez 48
Hadi Mapumziko: 0-0; Mashabiki waliohudhuria: 37,742

Reading           2 Jimmy Kebe 58, Noel Hunt 62                         
Newcastle United  2 Demba Ba 59,83                                      
Hadi Mapumziko: 0-0; Mashabiki waliohudhuria: 24,097

Everton           3 Leon Osman 25, Nikica Jelavic 32,37                 
Southampton       1 Gaston Ramirez 8                                    
Hadi Mapumziko: 3-1; Mashabiki waliohudhuria: 37,922

Fulham            1 Mladen Petric 10pen                                 
Manchester City   2 Sergio Aguero 43, Edin Dzeko 87                     
Hadi Mapumziko: 1-1; Mashabiki waliohudhuria: 25,698

Norwich City      2 Steve Morison 61, Grant Holt 87                     
Liverpool         5 Luis Suarez 2,38,57, Nuri Sahin 47, Steven Gerrard 68
Hadi Mapumziko: 0-2; Mashabiki waliohudhuria: 26,831

Stoke City        2 Peter Crouch 12,36                                  
Swansea City      0                                                     
Hadi Mapumziko: 2-0;  Mashabiki waliohudhuria: 27,330

Arsenal           1 Gervinho 42                                         
Chelsea           2 Fernando Torres 20, Juan Mata 53                    
Hadi Mapumziko: 1-1;  Mashabiki waliohudhuria: 60,101

No comments:

Post a Comment