MENEJA wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson amesema kuwa
muda wa dakika nne za nyongeza alizotoa mwamuzi wakati timu yake
ikifungwa Tottenham Hotspurs hazikuwa sahihi. Clint Dempsey ndiye
aliyefunga bao la ushindi na kuifanya Spurs kutoka na ushindi wa mabao
3-2 katika Uwanja wa Old Traford kwa mara ya kwanza katika kipindi cha
miaka 23. Ferguson amesema kuwa dakika nne za nyongeza zilizotolewa na
mwamuzi zilikuwa chache kutokana na Spurs kupoteza dakika nyingi katika
mchezo huo. Kocha huyo aliendelea kusema kuwa ni kitu kinachokatisha
tamaa kwasababu walikuwa na rekodi nzuri lakini anadhani mwamuzi
alichangia kuwafanya wapoteze mchezo huo baada ya kuongeza muda mchache
kulinganisha na ule ambao wapinzani walikuwa wakipoteza katika dakika
90. Hicho kinakuwa kipigo cha pili kwa United katika michezo sita ya
Ligi Kuu nchini Uingereza waliyocheza msimu huu ambapo sasa wanashika
nafasi ya tatu nyuma ya vinara wa ligi hiyo Chelsea na Everton.
Sir Alex Ferguson
Sir Alex Ferguson
No comments:
Post a Comment