BUKOBA SPORTS

Friday, September 7, 2012

US OPEN: DJOKOVIC ATINGA NUSU FAINALI.

 BINGWA mtetezi wa michuano ya wazi ya Marekani, Novak Djokovic amefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kumfunga Juan Martin del Porto kutoka Argentina. Djokovic raia wa Serbia ambaye anashika namba mbili katika orodha za ubora duniani kwa upande wa wanaume alifanikiwa kumfunga Del Porto kwa 6-2 7-6 6-4. Pamoja na kuwa chini ya kiwango katika michuano hiyo Djokovic ambaye ana umri wa miaka 25 amefanikiwa kushinda michezo yote bila kupoteza seti hata moja na sasa anatarajiwa kupambana na David Ferrer kutoka Hispania ili kutafuta nafasi ya kucheza fainali. Mshindi kati ya Djokovic na Ferrer atakutana na mshindi wa nusu fainali nyingine ambayo itawakutanisha Andy Murray wa Uingereza na Tomas Berdych wa Ujerumani.

No comments:

Post a Comment