>>FIFA yamleta kuangalia shughuli za Maendeleo ya Soka!
Nyota
wa zamani aw Ghana na klabu ya Olympique Marseille, Abedi Pele,
amewaambia Wachezaji chipukizi wa Tanzania kuwa "hakuna njia ya mkato
katika kutafuta mafanikio" na kuwataka kufanya jitihada ili watimize
ndoto, ikiwa ni pamoja na Serengeti Boys kuhakikisha inafuzu kucheza
Fainali za Afrika mwakani.
Pele, ambaye aliiongoza Marseille kutwaa
ubingwa wa Ulaya mwaka 1992 akifunga moja ya mabao dhidi ya AC Milan ya
Italia, alisema hayo Jana asubuhi wakati alipotembelea Kiti cha ufundi
cha Karume kushuhudia programu ya mazoezi ya vijana wadogo inayofanyika
kila misho wa wiki kwenye Uwanja wa Karume ambako watoto wa kuanzia umri
wa miaka sita hadi 17 hufundishwa mbinu za kusakata soka.
"Katika kufikia mafanikio hakuna njia ya
mkato," alisema Pele ambaye ameletwa nchini na Shirikisho la Kimataifa
la Vyama vya Mpira wa Miguu (FIFA) kuangalia shughuli mbalimbali za
maendeleo ya mpira wa miguu nchini.
"Tunaona wachezaji wenye vipaji vikubwa
duniani wakifanya jitihada kubwa ili waweze kucheza kwa kiwango cha juu.
Bila ya kufanya juhudi, kujituma na kudhamiria huwezi kufanikiwa.
"Wale wenye vipaji vikubwa, lakini
hawafanyi jitihada watabakia I. Wale wasiojaliwa kuwa na vipaji, lakini
wanafanya jitihada, watakwenda mbele na kupata mafanikio," alisema nyota
huyo ww Ghana ambaye alijijengea jina kwa kufunga mabao safi na muhimu
kwa nchi yake na klabu ya Olympique Marseille wakati ikitamba katika
soka barani Ulaya.
"Soka barani Afrika Lina mazingira
yanayofanana. Hakuna motto wa waziri anayecheza soka. Wala hakuna mtoto
wa mwanasheria au mfanyakazi ww benki ambaye anacheza soka. Soka
inachezwa na watu wanaotoka kwenye familia ambazo hazina maisha mazuri
na hivyo man nafasi sawa na wengine wote. Mnachotakiwa kufanya ni
kujituma, kudhamiria na kufanya jitihada ili mfungue mlango wa
mafanikio.
Pele, ambaye jina lake halisi ni Abedi
Ayew na ambaye watoto wake wainaichezea Marseille, pia aliwataka
wacheaji aw timu ya Taifa ya Vijana walio na umri china ya miaka 17
kufanya kila wawezalo ili wafuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika
zitakazofanyika Algeria mapema mwakani.
"Mkifuzu mtakuwa mmefungua milango ya
mafanikio ya maisha yenu," alisema gwiji huyo ambaye anaiwakilisha FIFA
katika kufuatilia programu mbalimbali za maendeleo. "nikiwaangalia naona
mna man uwezo wa kuwaondoa wapinzani wenu na nitafuatilia mechi yenu.
Mkifuzu tutakuwa wote na nitawaunga mkono.
Pele, ambaye kwa sasa anamiliki shule ya
mpira wa miguu ambayo imeshanikiwa kutwaa Kombe la FA mara moja,
ameambatana na Mkurugenzi wa Maendeleo wa FIFA kwa nchini za Kusini mwa
Afrika, Ashford Mamelodi na mmoja wa viongozi wa Idara ya Mawasiano ya
FIFA, Emmanuel, atakuwa nchini kwa siku tatu ambazo atazitumia kupata
taarifa za shughuli mbalimbali za maendeleo, zikiwemo za soka la watoto
(grassroots), soka la vijana, soka la wanawake na miradi mingine ya
maendeleo.
>>RIPOTI imesambazwa na Boniface Wambura,
AFISA HABARI TFF
No comments:
Post a Comment