Katika
Mechi mbili za Ligi Kuu England zilizochezwa leo, Liverpool na
Newcastle walitoka 1-1 na pia matokeo kuwa kama hayo kwa Mechi kati ya
QPR na Reading.
Liverpool 1vs Newcastle 1
Wakicheza kwao Uwanjani Anfield,
Liverpool wamefanikiwa kutoka sare ya Bao 1-1 na Newcastle ambao
walimaliza Mechi hii wakiwa Mtu 10 baada ya Sentahafu wao Fabricio
Coloccini kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu kwa rafu mbaya kwa Luis Suarez.
Newcastle ndio waliotangulia kupata bao
safi la Yohan Cabaye katika Dakika ya 43 lakini nae Luis Suarez
alisawazisha kwenye Dakika ya 67 pia kwa bao zuri.
Matokeo haya yamewaacha Newcastle
wakamate nafasi ya 10 wakiwa na Pointi 14 kwa Mechi 10 na Liverpool wapo
nafasi ya 12 wakiwa na Pointi 11 kwa Mechi 10.
Steven Gerrard receives an award from Gary McAllister to mark his 600th appearance
Wadau na wapenzi wa Liverpool walipata janga la bomba la maji hapa na kutokea mzozo wa hapa na pale
Suarez akishangilia huku akibusu mkono kama kawaida yake usiku huu baada ya kupata goli.
Nje, Coloccini is shown red card by ref Anthony Taylor
VIKOSI:
Liverpool: Jones, Wisdom, Skrtel, Agger, Jose Enrique, Gerrard, Allen, Sahin, Fernandez Saez, Suarez, Sterling
Akiba: Gulacsi, Assaidi, Henderson, Coates, Downing, Carragher, Shelvey.
Newcastle: Krul, Anita, Steven Taylor, Coloccini, Santon, Perch, Cabaye, Gutierrez, Ben Arfa, Cisse, Ba
Akiba: Harper, Simpson, Williamson, Shola Ameobi, Obertan, Sammy Ameobi, Ferguson.
Refa: Anthony Taylor
QPR 1 Reading 1
Dakika ya 66 Bao la Djibril Cisse likiwanyamazisha wapenzi wa soka na wadau wa Reading.
Sare hii haikuzisaidia Timu zote hizi mbili ambazo zipo mkiani na bado zinasaka ushindi wao wa kwanza kwenye Ligi Msimu huu.
Reading ndio walitangulia kupata Bao
katika Dakika ya 16 alilofunga Kaspars Gorkss baada ya kona ya Nicky
Shorey kuleta kizaazaa golini.
Kaspars Gorkss (katikati)baada ya dakika 16 wakishangilia na wenzake baada ya goli kupatikana
QPR walisawazisha katika Dakika ya 66 kwa Bao la Djibril Cisse.
Matokeo haya yanawaacha Reading wakamate
nafasi ya 18 wakiwa na Pointi 5 kwa Mechi 9 wakifuatiwa na QPR wenye
Pointi 4 kwa Mechi 10 na mkiani wapo Southampton wenye Pointi 4 kwa
Mechi 9.
Kiti cha Moto: Mkuu wa QPR Tony Fernandes, Mark Hughes na inaonekana kuna kukimbia kiti hapa.
Jamie Mackie (kushoto) akichuana na Sean Morrison
VIKOSI:
QPR: Julio Cesar, Bosingwa, Ferdinand, Nelsen, Traore, Mackie, Granero, Diakite, Taarabt, Hoilett, Cisse
Akiba: Green, Derry, Hill, Wright-Phillips, Onuoha, Zamora, Faurlin.
Reading: McCarthy, Gunter, Morrison, Gorkss, Shorey, McCleary, Leigertwood, Tabb, McAnuff, Roberts, Hunt
Akiba: Federici, Pearce, Pogrebnyak, Le Fondre, Kebe, Robson-Kanu, Cummings.
Refa: Michael Oliver
RATIBA MECHI ZIJAZO
Jumatatu, Novemba 5
[SAA 5 Usiku]
West Bromwich Albion v Southampton
Jumamosi, Novemba 10
[SAA 12 Jioni]
Arsenal v Fulham
Everton v Sunderland
Reading v Norwich City
Southampton v Swansea City
Stoke City v Queens Park Rangers
Wigan Athletic v West Bromwich Albion
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Aston Villa v Manchester United
Jumapili, Novemba 11
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Manchester City v Tottenham Hotspur
[SAA 12 Jioni]
Newcastle United v West Ham United
[SAA 1 Usiku]
Chelsea v Liverpool
No comments:
Post a Comment