BUKOBA SPORTS

Wednesday, November 14, 2012

AIRTEL YATOA MSAADA HOSPITALI YA RUFAA MUHIMBILI WODI YA WATOTO WANAOSUMBULIWA NA KANSA.


Mkurugenzi wa Mawasaliano wa Airtel bi Beatrice Singano Mallya(kulia) akikabidhi computer kwa Mkuu wa kitengo cha wodi ya watoto wanaougua Saratani kwa Daktari Sulende Kubhodja wa hospitali ya Muhimbili, (kati ni) Meneja wa jengo la wodi hiyo sista Judica Mwambo. Wafanyakazi wanawake wa Airtel Tanzania walitembelea hospitalini hapo mwishoni mwa wiki hii na kujitolea pia vifaa mbalimbali vikiwemo vitendea kazi vitakavyotumika kafanya usafi kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo Muhimbili

Mkurugenzi wa Mawasaliano wa Airtel bi Beatrice Singano Mallya (wapili kulia)akiongea na mmoja wa watoto waiolazwa katika hospitali ya Muhimbili mwishoni mwa wiki hii ambapo wafanyakazi wanawake wa Airtel waliamua kutembea watoto wenye kuugua Saratani katika Hospitali hiyo mwishoni mwa wiki hii, akifuwatiwa na Afisa uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde. Airtel ilijitolea vitu mbalimabli kwaajili ya hospitali hiyo ikiwemo computer, pamoja sabuni, miswaki, na dawa za meno kwaajili ya wagonjwa hao.

Wafanyakazi wanawake wa Airtel (Airtel Divas) wakiingia na mizigo yao katika wodi wa wagonjwa wanasumbuliwa na maradhi ya Saratani katika Hospitali ya Muhimbili, wafanyakazi hao walitembelea hospitalini hapo mwishoni mwa wiki hii na kujitolea pia vifaa mbalimbali vikiwemo vitendea kazi vitakavyotumika kafanya usafi kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo Muhimbili

Wafanyakazi wanawake wa Airtel Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaogua Saratani katika wodi ya Muhimbili walipowatembelea mwishoni mwa wiki hii ambapo Airtel walitoa misaada mbalimbali ikiwepo
komputa , sabuni, dawa za mswaki na mahitaji mengine muhimu.


DAR ES SALAAM, Tanzania

Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel kupitia programu yake ya AIRTEL DIVA imekabidhi misaada mbalimbali kwa wodi ya Watoto wanaougua maradhi ya Kansa katika Hospital ya Taifa Muhimbili. Ikiwa ni mchango toka kwa wafanyakazi wanawake wa Airtel kuunga mkono jitihada za Airtel katika kujitolea kwa jamii


Vifaa vilivokabidhiwa na wanafanyakazi hao wanawake wa Airtel Diva’s ni pamoja ma Kompyuta mpya kwaajili ya wodi hiyo, itakayotumika kutunza kumbukumbu za wagonjwa, pamoja na vifaa mbalimbali vikiwemo

vitendea kazi vitakavyotumika katika usafi kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo Muhimbili

Akizungumza Katika wakati wa kukabidhi Misaada hiyo,Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano,amesema kuwa utoaji misaada hiyo ni Mikakati thabiti iliyowekwa na kampuni hiyo katika kuhakikisha inakuwa karibu zaidi na jamii, sambamba na kutambua mchango wao katika kufanikisha jukumu zima la Biashara katika kipindi cha Mwaka mzima.


Singano amesema kuwa AIRTEL inatambua changamoto mbalimbali zinazoikabili Wodi ya Watoto wanaougua maradhi ya Kansa,na kubainisha kuwa Msaada walioutoa hautaishia hapo badala yake watakuwa wakifanya hivyo mara kwa mara katika Hospitali mbalimbali za ndani na nje ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Mawasiliano-Airtel Bi Beatrice Singano Airtel kupitia mpango wetu wa Diva, ambapo ni mkusanyiko wa wafanyakazi wote wanawake tumeona ni vyema kusaidiana na wazazi wenzetu kwa kuwapa pole namna hii, msaana huu tunaokabidhi leo tunaamini utagusa pia wadau wengine kuja kuwatembelea watoto na ndugu zetu wanaugua maradhi ya kansa katika hospital ya Muhimbili na hata zingine kwa lengo la kusaidiana Tumejionea wenyewe shida wanazopata ndugu zetu na hata wauguzaji hivyo tunaomba sana wanaweza kujitolea kuja kwa wingi na kuhakikisha tunasaidiana kwa hali na mali kunusuru maisha ya ndugu zetu hawa”alisema Bi Singano

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Watoto kutoka Hospital ya Taifa Muhimbili Dokta Surenda Kuboja, ameishukuru Kampuni ya AIRTEL kwa msaada walioutoa katika Wodi hiyo na kuyataka Makampuni mengine ya Kibiashara kuiga mfano uliuoonyeshwa na AIRTEL

Naye Meneja wa Jengo la Watoto kutoka Hospitalini hapo Bi Julitha Mbwambo amesema kuwa Watoto wanaotibiwa katika Wodi hiyo wamekuwa wakikabiliwa na Changamoto mbalimbali hivyo Misaada iliyotolewa na AIRTEL itawasaidia katika kupunguza matatizo mbalimbali yanayowakabili.

Nao baadhi ya Wazazi waliozungumza wodini hapo wamesema kuwa Watoto wanaowauguza wanahitaji faraja zaidi katika Maisha yao na kuyaomba makampuni mbalimbali kufuata nyayo za Airtel kwa kuwatembelea na

kuwafariji zaidi. Pia Zuwena Lisele Mzazi anayeuguza nae alisema “maisha ya hospitali ukiwa unauguza ni magumu sana kwa kuwa hakuna anaekuwa amejipanga kwaajili ya kukabiliana na changamoto za ugonjwa kwa wakati unapotokea, hivyo kwa niaba ya wenzangu wote ninawashukuru sana wanawake wenzagu
kutoka Airtel kwa kuliona hili na kuja kutoa pole hii, kwa kweli tumefarijika Airtel Diva ni mpango ulio chini ya wafanyakazi wote wanawake wa Airtel Tanzania wenye lengo la kuwaweka pamoja kujadili changamoto
mbalimbali za kijamii na kuzitolea ufumbuzi kwa lengo la kuimarishana.
Airtel Diva pia wanalengo la kuhakikisha wanatoka nje ya mazingira ya kazi na kuhudumia jamii kwa hali na mali ili kutatua changamoto mbalimbali zikiwemo kuchangia Afya, pamoja na kuelimisha moto wa kike na jamii kwa ujumla kutambua haki zao.

No comments:

Post a Comment