BUKOBA SPORTS

Tuesday, November 13, 2012

BALOZI WA KINYWAJI CHA HENNESSY AWASILI NCHINI


Balozi wa kinywaji cha Hennessy, Cyrille Gautier Auriol akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu utumiaji wa vinywaji vya kampuni hiyo katika ukanda wa Afrika Mashariki.



 

DAR ES SALAAM, Tanzania
 
BALOZI wa kinywaji cha Hennessy, Cyrile Gautier Auriol, amewasili nchini kwa dhumuni la kuelimisha na kujenga uelewa kuhusu utumiaji wa vinywaji vya kampuni hiyo katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Balozi huyo ambaye atakua nchini kwa muda wa siku mbili ikiwa ni katika ziara yake ya siku katika ukanda wa Afrika Mashariki pia atatoa mafunzo hayo kwa wahudumu mbalimbali wa bar kubwa mbalimbali hapa nchini.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo amesema kuwa elimu hiyo itatolewa nchi zote za Afrika Mashariki kwa lengo la kuwapa elimu juu ya uchanganyaji wa kinywaji hicho ili kuwaongezea uelewa katika ufanyaji wao wa kazi za kila siku.


Ameongeza kuwa baada ya ziara hiyo ataendelea kufanya ziara katika nchi zingine za ukanda huo kwa lengo la kuzidi kuhamasisha matumizi ya kinywaji hicho.


Ziara hiyo itahitimishwa na kuwaelimisha na kuwaburudisha wageni maalum wakiwemo wanamitindo maarufu na wafanyabiashara na pia atazindua chumba cha kinywaji hicho katika Club 327.


'Kutakua na kikao maalum na wapenzi wakubwa wa kinywaji hicho na kuwazawadia mialiko ya kuingia kwenye klabu ya wapenzi wa kinywaji hicho Afrika Mashariki' amesema balozi huyo.

No comments:

Post a Comment