BUKOBA SPORTS

Friday, November 30, 2012

CECAFA CHALLENGE CUP 2012: ZANZIBAR HEROES YAWAFURAHISHA WATANZANIA, YAICHAPA RWANDA WAKINA NIYONZIMA GOLI 2-1 KWENYE UWANJA ULIOJAA TOPE!

Zanzibar Heroes imetinga nusu fainali kwa kuifunga Rwanda jumla ya mabao 2-1 ambapo ingeweza kupata ushindi mnono zaidi kupitia kwa mshambuliaji wake Seif Abdalah nyota wa O.F.A . ambaye alipoteza nafasi kadhaa za kukwamisha mipira kimiani.

Ikiwa imeanza na wachezaji nane wanaocheza ligi kuu ya Tanzania Bara, timu ya Taifa ya Zanzibar ( Zanzibar Heroes) imeungana na timu za Uganda na Burundi, kufuzu kwa hatua ya robo fainali ya michuano ya 38 ya Tusker Challenge Cup.

Zanzibar iliweza kuonyesha soka la nguvu tofauti na walivyocheza mchezo wa ufunguzi dhidi ya Eritrea, jumatatu iliyopita. Ilitumia dakika nane tu kuandika bao lake la kuongoza.
Hamis Mcha Hamis, mtoto wa mwanasoka wa zamani wa Zanzibar na timu ya taifa ya Tanzania, alitumia makosa ya ‘ lazima’ za mlinda mlando wa Rwanda, Jean Claude Ndoli, ambaye aliukosa mpira uliokuwa umepigwa na kiungo-mshambuliaji wa pembeni, Suleiman Kassim Selembe, kutokana na kufanya kosa hilo, Mcha, alifunga bao la kwanza kwa nchi yake katika michuano hiyo. Zanzibar, ambao hawakuonekana kuathiriwa sana na hali ya uwanja wa Namboole, kujaa maji,
Rwanda 2-1 Zanzibar (Michuano iliyopita)

Mwadini Ally Mwadini, aliwapanga vyema walinzi wake, Nassorro Masoud, Nadir Haroub, Aggrey Morris, na Nuhu Samih, na kuibuka nyota wa mchezo, mara kadhaa alitumia mwili wake kuinusuru timu yake isipoteze mchezo, aliuwahi mpira uliokuwa umepigwa na kiungo wa Rwanda, Haruna Niyonzima, ukiwa unaelekea nyavuni, alifanya kazi kubwa katika nafasi yake na hilo lilipelekea jitihada za timu nzima kuzaa matunda. Zanzibar, walikwenda nusu ya kwanza ya mchezo wakiwa mbele kwa bao 1-0.

Waliingia kipindi cha pili wakiwa na tahadhali zaidi, nidhamu yao kama mchezaji mmoja mmoja ilikuwa juu, na kwa pamoja walielekezana kila penye mapungufu. Mchezo wao wa kupasiana haukuonekana sana sababu ya uwanja kutokuwa katika hali nzuri. Walijilinda vizuri, japo walinzi mara kadhaa walipitika, lakini uwezo mzuri wa Mwadini uliwahakikishia ushindi, zikiwa zimebaki dakika 20,Rashid Abdalah, aliifungia, Zanzibar, bao la pili. Baadae, Rwanda wakapata bao lao pekee.

Kwa matokeo hayo, Zanzibar, imekuwa timu ya kwanza kufuzu kwa robo fainali kutoka katika kundi C, na timu ya tatu kufuzu kwa hatua hiyo hadi sasa. Zanzibar, imefikisha pointi nne na kuziacha, Rwanda na Malawi, na pointi zao tatu, tatu, uku Eritrea ikiwa na pointi moja. Mechi za mwisho za kundi hili C, zitachezwa siku ya jumapili kwa Malawi kucheza na Zanzibar, uku, Rwanda ikiwakabili, Eritrea.
MABAO mawili ya Zanzibar yalifungwa na Kiungo wa Azam FC, Khamis Mcha ‘Vialli’ dakika ya 6 na 61, na la Rwanda limefungwa na Dadi Birori dakika ya 79.

MAKUNDI:
KUNDI A: Uganda, Ethiopia, Kenya, South Sudan
KUNDI B: Sudan, Tanzania, Burundi, Somalia
KUNDI C: Rwanda, Malawi, Zanzibar, Eritrea
Katika Mechi nyingine ya Kundi C, Malawi iliifunga Eritrea Bao 3-2 kwa Bao za Chiukepo Msowoya, Miciam Mhone na Patrick Masanjala na yale ya Eritrea kufungwa na Amir Hamad Omary na Yosief Ghide kwa penalti.
Michuano hii itaendelea Ijumaa Novemba 30 kwa Mechi za mwisho za Kundi A kwa Mechi za Kenya v Ethiopia na Uganda v South Sudan.

RATIBA/MATOKEO:
KUNDI A:
Novemba 24:  Ethiopia 1 South Sudan 0, Uganda 1 Kenya 0
Novemba 27: South Sudan 0 Kenya 2, Uganda 1 Ethiopia 0
Novemba 30: Kenya v Ethiopia,  South Sudan v Uganda

MSIMAMO:
[Kila Timu Mechi 2]
1 Uganda Pointi 6
2 Kenya 3 [Tofauti ya Magoli: 1]
3 Ethiopia 3 [Tofauti ya Magoli: 0]
4 South Sudan 0

KUNDI B:
Novemba 25: Burundi 5 Somalia 1, Tanzania 2 Sudan 0
Novemba 28: Somalia 0 Sudan 1, Tanzania 0 Burundi 1
Desemba 1: Sudan v Burundi, Somalia v Tanzania

MSIMAMO:
[Kila Timu Mechi 2]
1 Burundi Pointi 6
2 Kili Stars 3 [Tofauti ya Magoli: 1]
3 Sudan 3 [Tofauti ya Magoli: -1]
4 Somalia 0

KUNDI C:
Novemba 26: Zanzibar 0 Eritrea 0, Rwanda 2 Malawi 0
Novemba 29: Malawi 3 Eritrea 2, Rwanda 1 Zanzibar 2
Desemba 1: Malawi v Zanzibar, Eritrea v Rwanda

MSIMAMO:
[Kila Timu Mechi 2]
1 Zanzibar Pointi 4
2 Rwanda 3 [Tofauti ya Magoli: 1]
3 Malawi 3 [Tofauti ya Magoli: -1]
3 Eritrea 1

KUMBUKA.
ROBO FAINALI: Desemba 3 & 4
NUSU FAINALI: Desemba 6
FAINALI: Desemba 8

No comments:

Post a Comment