CHELSEA
Kocha wa muda wa Chelsea, Rafael
Benitez, ametangaza Kikosi kikali kwa ajili ya Michuano ya kuwania Taji
la FIFA la Klabu Bingwa Duniani ambayo wao wataanza kucheza hatua ya
Nusu Fainali dhidi ya Mshindi kati ya Bingwa wa Barani Asia, Usain
Hyundai kutoka Korea na Monterrey, ambao ni Mabingwa wa Marekani ya Kati
na Kaskazini.
Kikosi cha Chelsea kina Majina yote
makubwa wakiwemo Nahodha wao John Terry na Frank Lampard ambao wote bado
wamo kwenye Listi yao ya sasa ya Majeruhi wao.
Meneja Rafael Benitez ana uzoefu mkubwa
kwenye Mashindano ya Klabu Bingwa Duniani kwani hii itakuwa mara yake ya
3 kushiriki ambapo aliipeleka Liverpool Mwaka 2005 na kutolewa Fainali
na 2010, aliiongoza Inter Milan, iliyofikishwa huko na Jose Mourinho,
kutwaa Ubingwa wa Dunia.
KIKOSI KAMILI:
Makipa: Petr Cech, Ross Turnbull, Hilario
Mabeki: Branislav Ivanovic, Ashley Cole, David Luiz, Paulo Ferreira, Gary Cahill, John Terry, Cesar Azpilicueta, Ryan Bertrand
Viungo: Oriol Romeu, Ramires, Frank Lampard, Oscar, John Obi Mikel, Eden Hazard, Marko Marin, Lucas Piazon
Mafowadi: Fernando Torres, Juan Mata, Victor Moses, Daniel Sturridge
MCHEZAJI BORA 2012 - SHINJI KAGAWA!
Kiungo wa Japan na Manchester United Shinji Kagawa ametwaa Tuzo ya kwanza kabisa kutolewa na Shirikisho la Soka
Barani Asia, AFC, ya Mchezaji Bora wa Mwaka 2012 kwa Wachezaji wa
Kimataifa, wale wanaocheza nje ya Asia.
Katika kutwaa Tuzo hiyo Shinji Kagawa
aliwashinda Yuto Nagatomo wa Japan anaecheza Klabu ya Inter Milan na
Kipa Veterani wa Australia anaechezea Fulham, Mark Schwarzer.
Washindi hao walitajwa huko Kuala Lumpur, Malaysia hii leo.
Mchezaji wa Korea ya Kusini, anaechezea
Klabu Bingwa ya Asia, Lee Keun-ho, ndie Mchezaji Bora kwa Wachezaji
wanaocheza ndani ya Asia.
Lee aliwashinda Kiungo wa Iran Ali Karimi na Beki wa China Zheng Zhi.
Katika Tuzo nyingine mpya anayozawadiwa
Mchezaji wa kutoka nje ya Asia anaecheza Asia Mshindi ni Mbrazil Rogerio
De Assis Silva Coutinho wa Klabu ya United Arab Emirates Al Jazira.
KLABU BINGWA DUNIANI 2012
TIMU ZITAKAZOSHIRIKI:
Chelsea-BINGWA ULAYA
Corinthians-BINGWA MAREKANI ya KUSINI
Monterrey-BINGWA MAREKANI ya KATI NA KASKAZINI
Auckland City-BINGWA KANDA ya OCEANIA
Usain Hyundai-BINGWA-Barani Asia
Al Ahly-BINGWA-Barani Afrika
Sanfrecce Hiroshima-BINGWA-Japan J-LIGI
RATIBA:
Raundi ya Mchujo - Desemba 6, Yokohama
1 Sanfrecce Hiroshima v Auckland City
ROBO FAINALI - Desembar 9, Toyota
2 Usain Hyundai v Monterrey
3 MSHINDI Mechi Na 1 v Al Ahly
MSHINDI wa 5- Desemba 12, Toyota
Aliefungwa Robo Fainali 1 v Aliefungwa Robo Fainali 2
NUSU FAINALI
Desemba 12, Toyota
5 Mshindi Mechi Na 3 v Corinthians
Desemba 13, Yokohama
6 Mshindi Mechi Na 2 v Chelsea
MSHINDI wa 3 - Desemba 16, Yokohama
FAINALI - Desemba 16, Yokohama
No comments:
Post a Comment