BUKOBA SPORTS

Tuesday, November 27, 2012

CECAFA TUSKER CUP: KILIMANJARO STARS VS BURUNDI.

TIMU ya taifa ya Tanzania Bara-Kilimanjaro Stars inasubiri kutupa karata yake nyingine kesho wakati itakapopambana na Burundi katika mchezo wa michuano ya Kombe la Tusker ambalo linaandaliwa na Baraza la Michezo kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati-CECAFA. Katika mchezo wa kwanza Kilimanjaro Stars ilifanikiwa kuisambaratisha Sudan kwa kuifunga mabao 2-0 hivyo kama wakishinda mchezo dhidi ya Burundi watakuwa wamejihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo. Kocha wa Kilimanjaro stars Kim Poulsen amesema kuwa maandalizi kwa ajili ya mchezo dhidi ya Burundi ambao waliifunga Somalia mabao 5-1 yamekamilika na ana uhakika kuwa ataibuka na ushindi kwenye mchezo huo. Poulsen alitamba kuwa kikosi chake ambacho kimesheheni wachezaji vijana kitafanya vizuri katika michuano hiyo na pia aliwasifu washambuliaji wake Mrisho Ngassa na John Bocco kwa kucheza kwa kuelewana na kuipa ushindi timu hiyo katika mchezo kwanza.

RATIBA/MATOKEO
KUNDI A:
Novemba 24:  Ethiopia 1 South Sudan 0, Uganda 1 Kenya 0
Novemba 27: South Sudan 0 Kenya 2, Uganda 1 Ethiopia 0
Novemba 30: Kenya v Ethiopia, South Sudan v Uganda

KUNDI B:
Novemba 25: Burundi 5 Somalia 1, Tanzania 2 Sudan 0
Novemba 28: Somalia v Sudan, Tanzania v Burundi
Desemba 1: Sudan v Burundi, Somalia v Tanzania

KUNDI C:
Novemba 26: Zanzibar 0 Eritrea 0, Rwanda 2 Malawi 0
Novemba 29: Malawi v Eritrea, Rwanda v Zanzibar
Desemba 1: Malawi v Zanzibar, Eritrea v Rwanda

No comments:

Post a Comment