BUKOBA SPORTS

Tuesday, November 6, 2012

CHRISTIANO RONALDO ACHOSHWA KUFANANISHWA NA MESSI!, BALLON d'Or.

>>AKIRI: “Uhasama na Messi ni wa Wanahabari!
Cristiano Ronaldo, akikiri kuwa kinyang’anyiro cha kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani- Ballon d'Or-kiko wazi na Mshindi anaweza kuwa yeyote, amesema amechoshwa na kushindanishwa na kufananishwa na Lionel Messi.
Wote, Ronaldo na Messi, wapo kwenye Listi ya Wachezaji 23 wanaogombea Ballon d'Or.
Alipohojiwa na Gazeti la France Footbal, ambalo pamoja na FIFA ndio Waandaaji wa Tuzo hiyo, Ronaldo alipoza uhasama na Messi na pia kukiri wapo wengi wanaoweza kutwaa Tuzo hiyo.
Alisema: “Uhasama na Messi ni wa Wanahabari. Kila mara tunauona ili Watu wauze Magazeti na kuvutia Watazamaji wa TV.”
Aliongeza: “Ukweli kuwa nimechoshwa na hilo. Ni mzigo lakini mizoea. Sipendi kujilinganisha na wengine.”Ronaldo alimalizia: “Messi anaweza kutwaa Ballon d'Or na vile vile Xavi au Iniesta. Na tusiwasahau Drogba au Falcao. Wanaweza kutwaa Tuzo.”
Washindi wa Tuzo ya Ballon d'Or hupatikana kwa Kura za Mameneja wa Timu za Taifa na Manahodha wao pamoja na Kundi maalum la Wanahabari.
Kabla ya Mshindi kutangazwa hapo Januari 7, Listi hiyo ya Wachezaji 23 itapunguzwa na kuwa Wagombea watatu tu.

LISTI YA WACHEZAJI BORA:
-Sergio Aguero (Manchester City/Argentina),
-Xabi Alonso (Real Madrid/Spain),
-Mario Balotelli (Manchester City/Italy),
-Karim Benzema (Real Madrid/France),
-Gianluigi Buffon (Juventus/Italy),
-Sergio Busquets (Barcelona/Spain),
-Iker Casillas (Real Madrid/Spain),
-Cristiano Ronaldo (Real Madrid/Portugal),
-Didier Drogba (Shanghai Shenhua/Ivory Coast),
-Radamel Falcao (Atletico Madrid/Colombia),
-Zlatan Ibrahimovic (Paris St Germain/Sweden),
-Andres Iniesta (Barcelona/Spain),
-Lionel Messi (Barcelona/Argentina),
-Manuel Neuer (Bayern Munich/Germany),
-Neymar (Santos/Brazil),
-Mesut Ozil (Real Madrid/Germany),
-Gerard Pique (Barcelona/Spain),
-Andrea Pirlo (Juventus/Italy),
-Sergio Ramos (Real Madrid/Spain),
-Wayne Rooney (Manchester United/England),
-Yaya Toure (Manchester City/Ivory Coast),
-Robin van Persie (Manchester United/Netherlands),
-Xavi (Barcelona/Spain)

No comments:

Post a Comment