BUKOBA SPORTS

Tuesday, November 6, 2012

SIR ALEX FERGUSON MENEJA BORA WA MWEZI, KWAKE NI REKODI YA 27, ANAFUATIA MZEE WENGER MARA 12

Sir Alex Ferguson wa Manchester United ameteuliwa ndiye Meneja Bora wa Ligi Kuu England kwa Mwezi Oktoba na hii ni mara yake ya 27 kutwaa Tuzo hiyo na kumfanya awaache kwa mbali Mameneja wenzake waliowahi kutwaa Tuzo hiyo huku anayemfuata ni Arsene Wenger wa Arsenal alietwaa mara 12 tu.
Kwa upande wa Wachezaji alietwaa Tuzo ya Mchezaji Bora kwa Mwezi Oktoba ni Juan Mata.
Sir Alex Ferguson, ambae baadae Mwezi huu atatimiza Miaka 26 ya utumishi akiwa na Man United, ametunukiwa Tuzo hii kwa kuiongoza Man United Mwezi Oktoba na kufunga jumla ya Mabao 10 walipopata ushindi dhidi ya Newcastle, Stoke City na Chelsea.

TUZO YA MENEJA BORA WA LIGI KUU ENGLAND:
1 Alex Ferguson Mara 27
2 Arsene Wenger 12
3 David Moyes 9
4 Martin O’Nell 8
5 Harry Redknapp 8
6 Bobby Robson 6
7 Rafael Nenitez 5
8 Kevin Keegan 5

Akiongea baada ya kuteuliwa, Sir Alex Ferguson alisema: “Nafurahia uchezaji wetu wa kushambulia, hiyo ndio alama yetu. Tumekuwa na kasoro kwenye Difensi lakini kwenye Mechi na Arsenal niliona ninachotegemea kwa Mabeki wa Man United.”
HONGERA SANA MZEE FERGIE, BUKOBASPORTS INAKUTAKIA MAFANIKIO MEMA!!!!

No comments:

Post a Comment