BUKOBA SPORTS

Wednesday, November 14, 2012

DJONKOVIC AMSHINDA FEDERER - ATP

Novak Djonkovic
Mchezaji nambari moja duniani, katika mchezo wa Tennis kwa upande wa wanaume, Novak Djonkovic, amesema ushindi wake katika fainali ya mashindano ya ATP yaliyomalizika mjini London, ni afueni na ushindi kwa babake ambaye anaugua.
Mchezaji huyo kutoka Serbia, alimshinda Rogger Federr kwa seti mbili kwa mbila za 7-6(8-6) na 7-5 kushinda fainali hiyo iliyochezwa katika ukumbi wa O2 Arena.
Baada ya ushindi huo, Djonkovic, alisema alipewa motisha na babake Srdjan, ambaye anasemekana anauguza maradhi ya pumu.
Amekiri kuwa mafanikio yake ya kumaliza msimu katika nafasi ya kwanza mwaka huu, yamewiana na matokeo yake ya mwakwa uliopita ambapo pia alishinda mataji matatu kati ya nne nakuandikisha historia ya kutoshindwa katika mechi 43.
Wakati wa mechi hiyo kali, Djokovic alizidiwa nguvu mara kadhaa na mpinzani wake, lakini alijikakamua na kutoka nyuma na kumshinda Federer, katika mechi hiyo iliyodumu kwa saa mbili na dakika kumi na nne.

No comments:

Post a Comment