BUKOBA SPORTS

Sunday, November 11, 2012

ENGLISH PREMIER LEAGUE: CHELSEA 1 vs LIVERPOOL 1. CHESEA WASHUKA HADI NAFASI YA TATU!


Wakiwa kwao  Chelsea leo wamelazimishwa sare ya goli 1 kwa 1 na timu ya Liverpool.
Nahodha John Terry akiichezea Mechi yake ya kwanza ya Ligi tangu afungiwe Mechi 4 aliifungia Chelsea bao moja lakini Liverpool walizinduka na kusawazisha kupitia Luis Suarez na Mechi kumalizika 1-1 na kuwafanya Chelsea waipishe Man City kwenye nafasi ya pili wakiwa nyuma ya vinara Manchester United.
John Terry akiifunga timu yake goli kwa kichwa

MSIMAMO NANE ZA JUU
1 Man United Mechi 11 Pointi 27
2 Man City  Mechi 11 Pointi 25
3 Chelsea Mechi 11 Pointi 24
4 Everton Mechi 11 Pointi 20
5 WBA Mechi 11 Pointi 20
6 West Ham Mechi 11 Pointi 18
7 Tottenham Mechi 11 17
8 Arsenal Mechi 11 Pointi 16
John Terry akichukuliwa nje ya uwanja kwa matibabuJohn Terry akilalamika baaada ya kupata maumivu muda mchache baada ya kulaliwa mguu na Suarez

Jamie Carragher (kulia) akichuana na striker Fernando Torres usiku huu.

Suarez akiwaacha hoi Chelsea dakika ya 73 baada ya kutupia goli la kusawazisha.


VIKOSI:
Chelsea: Cech, Azpilicueta, Terry, Ivanovic, Bertrand, Mikel, Ramires, Hazard, Oscar, Mata, Torres
Akiba: Turnbull, Romeu, Moses, Ferreira, Marin, Sturridge, Cahill.
Liverpool: Jones, Wisdom, Carragher, Agger, Johnson, Allen, Gerrard, Sterling, Sahin, Jose Enrique, Suarez
Akiba: Gulacsi, Cole, Assaidi, Henderson, Coates, Downing, Fernandez Saez.
Refa: Howard Webb


RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumamosi, Novemba 17, 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Arsenal v Tottenham Hotspur
[SAA 12 Jioni]
Liverpool v Wigan Athletic
Manchester City v Aston Villa
Newcastle United v Swansea City
Queens Park Rangers v Southampton
Reading v Everton
West Bromwich Albion v Chelsea
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Norwich City v Manchester United

No comments:

Post a Comment