MANCHESTER, England
KOCHA Sir Alex Ferguson, ameshawishika kuamini kuwa, kikosi chake cha Manchester United kitafanya makubwa msimu huu wa Ligi Kuu, ikiwamo kutikisa nyavu mara 100 katika mechi tofauti za ligi hiyo.
Rekodi ya karibu kwa Fergie kufikisha idadi hiyo ilikuwa ni msimu wa 1999/2000, wakati Mashetani Wekundu walipofunga jumla ya mabao 97 na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwa tofauti ya pointi 18 dhidi ya Arsenal.
Tambo za Fergie msimu huu zimekuja wakati klabu hiyo ikiwa imefunga mabao kadhaa kupitia wachezaji 13 tofauti, huku Robin van Persie akiongoza kwa mabao yake 11 katika mechi 14 za mashindano tofauti.
Mabao manane ya Mholanzi huyo katika mechi nane alizoanzishwa katika Ligi Kuu, yameifanya Man United kufunga jumla ya mabao 26 - kabla ya pambano lao la jana Jumamosi dhidi ya Aston Villa kwenye Uwanja wa Villa Park.
Fergie anasisitiza kuwa, kikosi chake kina uwezo wa kuimarika kila uchao na kuwezesha kufunga mara tatu zaidi ya hayo.
Akasema kuwa: “Jambo la kufarahisha kwangu ni kuzidi kutikisa nyavu zaidi na zaidi kwa kila timu itakayokatiza mbele yetu. Kuwa na wafungaji tofauti 13 hadi sasa, ni jambo linalotupa nguvu ya ziada katika mechi zetu.
“Tuna mabeki kama Evans na Evra ambao tayari wameshafunga mabao mawili kila mmoja na kuwa mara mbili zaidi ki-utendaji wao. Lakini pia tutapata kutoka kwa kila mmoja miongoni mwao ama mwingine,” alisema Fergie
No comments:
Post a Comment