>>RVP kuivaa Timu yake ya zamani kwa MARA ya KWANZA!!
>>PATA DONDOO na REKODI za Mechi Man United v Arsenal!
Ligi Kuu England, BPL [Barclays Premier
League], inaingia kwenye Raundi yake ya 10, isipokuwa kwa Sunderland na
Reading ambazo zina kiporo cha Mechi kati yao, na baada ya Wikiendi
iliyopita vinara Chelsea kunyukwa bao 3-2 wakiwa kwao Stamford Bridge na
Manchester United, lile pengo kati ya Chelsea na Timu za nyuma yake,
Man United na Mabingwa Man City, limebaki Pointi 1 tu.
Mbali ya Man United ambao wako nyumbani
kupambana na Arsenal katika Mechi ya kwanza kabisa hapo Jumamosi,
Chelsea na Man City zote zipo ugenini kwa Chelsea kucheza na Swansea
City na Man City kukipiga na West Ham huko Upton Park, Jijini London.
Kufuatia Chelsea kuwasilisha malalamiko
kwa FA, Chama cha Soka England, kuhusu Refa Mark Clattenburg kutumia
lugha isiyofaa katika Mechi Chelsea waliyofungwa 3-2 na Manchester
United Jumapili iliyopita dhidi ya Wachezaji wake John Mikel Obi na Juan
Mata na pia kuwepo kwa uchunguzi wa Polisi baada ya Kikundi cha
Wanasheria Weusi kulalamika kuhusu tukio hilo, Refa huyo ameondolewa
kuchezesha Mechi za Wikiendi hii.
Jumamosi Novemba 3, ndani ya Uwanja wa
Old Trafford, Manchester United itaikaribisha Arsenal katika moja ya
Mechi za Ligi Kuu England, BPL, ambayo inangojewa kwa hamu kubwa kwani
inazikutanisha Timu ambazo, kati yao, zimefunga na kufungwa jumla ya
Magoli 41 katika Mechi 8 kuanzia Oktoba 20 na pia mvuto upo kumuona
Nahodha wa zamani wa Arsenal, Robin van Persie, akiivaa Klabu yake ya
zamani kwa mara ya kwanza tangu ahamie Man United mwanzoni mwa Msimu
huu.
Bila shaka, Arsenal watakuwa na wasiwasi
kumvaa Straika ambae wakiwa nae Msimu uliopita aliifungia jumla ya
Magoli 37 na tangu atue Man United mtambo wake wa magoli umeendelea
mtindo mmoja.
Juzi Jumanne, Arsenal walitoka nyuma kwa
Bao 4-0 walipocheza kwenye Kombe la Ligi na kuifunga Reading 7-5 katika
Dakika 120 za Mchezo huku Theo Walcott akipiga hetitriki.
MSIMAMO TIMU ZA JUU.
[Kila Timu imecheza Mechi 9]
1 Chelsea Pointi 22
2 Man United 21 [Tofauti ya Magoli 11]
3 Man City 21 [Tofauti ya Magoli 9]
4 Tottenham 17
5 Everton 16
6 Arsenal 15
7 Fulham 14
8 WBA 14
9 West Ham 14
10 Newcastle 13
Msimu uliopita, Mwezi Agosti Mwaka jana
Uwanjani Old Trafford, Arsenal walichabangwa bao 8-2 kwenye Mechi ya
Ligi na Msimu huu Man United wamekuwa wakiendeleza wimbi lao la kufunga
Mabao mengi kila Mechi baada ya Jumapili iliyopita kushusha kipigo cha
kwanza kwenye Ligi kwa vinara wa Ligi Chelsea Uwanjani Stamford Bridge
walipoifunga 3-2 lakini Siku 3 baadae, Jumatano, Chelsea walilipa kisasi
kwa kuifunga Man United, iliyochezesha Kikosi cha Pili, bao 5-4,
kwenye Mechi ya Kombe la Ligi iliyochukua Dakika 120 baada ya kutoka 3-3
katika Dakika 90.
Katika Mechi 8 za mwisho kucheza Old
Trafford, Arsenal hawajashinda hata moja baada ya kuchapwa na Man United
katika Mechi 7 kati ya hizo na sare 1 tu.
Kimsimamo kwenye Ligi, Arsenal wapo
nafasi ya 6 wakiwa na Pointi 15 na Man United wapo nafasi ya pili,
Pointi moja nyuma ya vinara Chelsea, na wana Pointi 21.
HAPO HAPO, WENGER ANAKILI KUWA VAN PERSIE NI "MOTO"
-ITAKUWA NI MECHI YA KWANZA KWA ROBIN VAN PERSIE TANGU AIHAME!!
Arsene Wenger amepoza maneno ya Mashabiki wa Arsenal kutaka kisasi kwa Robin van Persie kwa kuihama
Timu hiyo na kwenda Manchester United wakati Timu hizo zitakapokutana
Jumamosi Uwanjani Old Trafford kwenye Mechi ya Ligi Kuu England na hiyo
ikiwa mara ya kwanza kwa Nahodha huyo wa zamani wa Arsenal kukutana na
Timu yake ya zamani tangu ahame.
Wenger amewataka Mashabiki wa Arsenal
watakaokuwepo Old Trafford kumwonyeshea heshima Robin van Persie na si
kumkashifu na kumtukana.
Wenger alitamka: “Kwetu, muhimu ni
matokeo na uchezaji wetu. Hatumzunguzii kabisa Van Persie. Natumaini
Mashabiki watamuheshimu kwani kachezea kwetu Miaka minane na alifanya
vizuri sana!”
Alihoji: “Tunapiga vita Ubaguzi, Wiki iliyopita ilikuwa hivyo na kwa nini isiwe sasa?”
Akiichezea Arsenal, Robin van Persie,
mwenye Miaka 29, aliifungia Arsenal jumla ya Mabao 132, 37 yakiwa Msimu
uliopita na kuwawezesha kushika nafasi ya 3 kwenye Ligi.
Wenger amesema: “Daima unataka uongoze
Watu vizuri wawe na maisha mazuri! Wakifanikiwa unaridhika, sidhani
kwake nilifanya vibaya!”
Hadi sasa, kwa Kipindi kifupi, Van
Persie ameifungia Man United Bao 7 kwenye Ligi na yeye na Demba Ba wa
Newcastle ndio wanaongoza kwenye Ufungaji.
Hilo halikumshangaza Wenger ambae
ametamka: “Sishangazwi na yeye kufanya vizuri. Man United ina Wachezaji
wazuri sana, na Robin ni mjanja kwenye boksi, mwenye kasi na kujua
nafasi huashangaza! Wapo Wachezaji wazuri na Robin atanufaika tu. Robin
ni Straika hatari sana!”
USO kwa USO -Man United v Arsenal:
WAMECHEZA JUMLA MECHI: 214
-Arsenal: Ushindi: 78
-Man United: Ushindi 90
-Sare: 46
NYUMBANI kwa Arsenal: Mechi 101
-Arsenal: Ushindi: 57
-Man United: Ushindi 27
-Sare: 17
NYUMBANI kwa Man United: Mechi 102
-Man United: Ushindi 60
-Arsenal: 17
-Sare: 25
MATOKEO Misimu ya hivi karibuni:
2011/12:
Januari 22-Arsenal 1 Man United 2 [BPL]
Agosti 28-Man United 8 Arsenal 2 [BPL]
2010/11:
Mei 1-Arsenal 1 Man United 0 [BPL]
Machi 12-Man United 2 Arsenal 0 [FA Cup]
Desemba 13-Man United 1 Arsenal 0 [BPL]
2009/10
Januari 31-Arsenal 1 Man United 3 [BPL]
Agosti 29-Man United 2 Arsenal 1 [BPL]
2008/9:
Mei 16-Man United 0 Arsenal 0 [BPL]
Mei 5-Arsenal 1 Man United 3 [UEFA CHAMPIONZ LIGI]
Aprili 29-Man United 1 Arsenal 0 [UEFA CHAMPIONZ LIGI]
Novemba 8-Arsenal 2 Man United 1 [BPL]
2007/8:
Aprili 13-Man United 2 Arsenal 1 [BPL]
Februari 16-Man United 4 Arsenal 0
Novemba 3-Arsenal 2 Man United 2
REKODI-Mabao Mengi:
-2011/12: Man United 8 Arsenal 2
-1946/47: Arsenal 6 Man United 2
ZIFUATAZO NI RATIBA, MSIMAMO, MAREFA waliopangwa Mechi zote za Wikiendi na WAFUNGAJI BORA:
RATIBA:
Jumamosi, Novemba 3, 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Manchester United v Arsenal
[SAA 12 Jioni]
Fulham v Everton
Norwich City v Stoke City
Sunderland v Aston Villa
Swansea City v Chelsea
Tottenham Hotspur v Wigan Athletic
[SAA 2 na Nusu Usiku]
West Ham United v Manchester City
Jumapili, Novemba 4, 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Queens Park Rangers v Reading
[SAA 1 Usiku]
Liverpool v Newcastle United
Jumatatu, Novemba 5, 2012
[SAA 5 Usiku]
West Bromwich Albion v Southampton
MAREFA wa MECHI za WIKIENDI:
Jumamosi Novemba 3
Manchester United v Arsenal
Refa: M Dean
Wasaidizi: S Ledger, A Garratt
Refa wa Akiba: P Dowd
Fulham v Everton
Refa: N Swarbrick
Wasaidizi: D Bryan, M Wilkes
Refa wa Akiba: M Oliver
Norwich City v Stoke City
Refa: A Marriner
Wasaidizi: G Beswick, A Holmes
Refa wa Akiba: P Tierney
Sunderland v Aston Villa
Refa: M Jones
Wasaidizi: D C Richards, J Brooks
Refa wa Akiba: C Foy
Swansea City v Chelsea
Refa: K Friend
Wasaidizi: C Breakspear, M Scholes
Refa wa Akiba: J Moss
Tottenham Hotspur v Wigan Athletic
Refa: M Atkinson
Wasaidizi: S Child, M McDonough
Refa wa Akiba: C Pawson
West Ham United v Manchester City
Refa: H Webb
Wasaidizi: D Cann, P Bankes
Refa wa Akiba: L Mason
Jumapili Novemba 4
Queens Park Rangers v Reading
Refa: M Oliver
Wasaidizi: S Long, D England
Refa wa Akiba: M Atkinson
Liverpool v Newcastle United
Refa: A Taylor
Wasaidizi: S Burt, A Halliday
Refa wa Akiba: M Jones
Jumatatu Novemba 5
West Bromwich Albion v Southampton
Refa: M Halsey
Wasaidizi: R Ganfield, J Flynn
Refa wa Akiba: M Dean
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 9 isipokuwa inapotajwa]
1 Chelsea Pointi 22
2 Man Utd 21
3 Man City 21
4 Tottenham 17
5 Everton 16
6 Arsenal 15
7 Fulham 14
8 West Brom 14
9 West Ham 14
10 Newcastle 13
11 Swansea 11
12 Liverpool 10
13 Stoke 9
14 Sunderland Mechi 8 Pointi 9
15 Wigan 8
16 Norwich 7
17 Aston Villa 6
18 Reading Mechi 8 Pointi 4
19 Southampton 4
20 QPR 3
WAFUNGAJI BORA:
Demba Ba [Newcastle] Mabao 7
Van Persie [Man United] 7
Michu [Swansea] 6
Suarez [Liverpool] 6
Defoe [Tottenham] 5
Dzeko [Man City]5
Fletcher [Sunderland] 5
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumamosi, Novemba 10, 2012
[SAA 12 Jioni]
Arsenal v Fulham
Everton v Sunderland
Reading v Norwich City
Southampton v Swansea City
Stoke City v Queens Park Rangers
Wigan Athletic v West Bromwich Albion
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Aston Villa v Manchester United
Jumapili, Novemba 11, 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Manchester City v Tottenham Hotspur
[SAA 12 Jioni]
Newcastle United v West Ham United
[SAA 1 Usiku]
Chelsea v Liverpool
No comments:
Post a Comment