BUKOBA SPORTS

Wednesday, November 7, 2012

VODA PREMIER LEAGIE: AZAM 1 vs JKT OLJORO O, COASTAL UNION 1 vs POLISI MORO O, MTIBWA SUGAR 1 vs JKT RUVU 0 - SIMBA YASHUKA NAFASI YA 3!.


MATOKEO:
Jumatano Novemba 7
Azam 1 JKT Oljoro 0
Coastal Union 1 Polisi Moro 0
Mtibwa Sugar 1 JKT Ruvu 0

Wakiwa kwao Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam, leo Azam FC wamefuta machungu ya kulambishwa Bao 2-0 na Yanga kwa kuwafunga JKT Oljoro Bao 1-0 katika Mechi ya Ligi Kuu Vodacom, VPL, kwa Bao la Mchezaji wao kutoka Ivory Coast, Kipre Tchetche.

MSIMAMO TIMU ZA JUU
1 Yanga Mechi 12 Pointi 26
2 Azam FC Mechi 12 Pointi 24
3 Simba Mechi 12 Pointi 23
4 Coastal Mechi 12 Pointi 22

Bao hilo la Tchetche, aliefunga kwa Penati, limewafanya Azam wakamate nafasi ya pili na kuwashusha Mabingwa watetezi Simba hadi nafasi ya 3.
Yanga bado wako kileleni wakiwa na Pointi 26.
Kwenye Mechi nyingine za Ligi zilizochezwa leo, huko Mkwakwani, Tanga, Coastal Union wameifunga Polisi Morogoro Bao 1-0 kwa bao la Daniel Lyanga na huko Manungu, Morogoro, Mtibwa Sugar nao pia wameishinda JKT Ruvu kwa Bao 1-0 kwa bao la Issa Rashid.

RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumamosi Novemba 10
Mgambo JKT v Azam (Mkwakwani, Tanga)
African Lyon v Mtibwa Sugar (Azam Complex, Dar es Salaam)
Jumapili Novemba 11
Simba v Toto Africans (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam)
Coastal Union v Yanga (Mkwakwani, Tanga)
Tanzania Prisons v JKT Ruvu (Sokoine, Mbeya)
Kagera Sugar v Polisi Morogoro (Kaitaba, Kagera)
JKT Oljoro v Ruvu Shootings (Sheikh Amri Abeid, Arusha)


MECHI ZA VIPORO VYA PRISONS:
Jumatano Novemba 14
Mgambo JKT v Tanzania Prisons [Mkwakwani, Tanga]
Jumapili Novemba 18
Ruvu Shooting v Tanzania Prison [Mabatini, Pwani]

No comments:

Post a Comment