Winga Mshambuliaji wa Tanzania MRISHO NGASSA ndiye aliyekuwa mwiba mkali kwa walinzi wa SOMALIA baada ya kuvunja rekodi ya michuano hiyo kwa kufunga mabao MATANO na mabao MAWILI yakifungwa JOHN BOCCO.
Nayo timu ya ZANZIBAR imefungwa mabao mawili kwa bila dhidi ya MALAWI ,wakati timu ya RWANDA ikiibuka na ushindi wa mabao MAWILI kwa bila dhidi ya ERITREA na BURUNDI ikiifunga SUDAN bao moja kwa bila.
Robo fainali ya michuano hiyo itaendelea jumatatu kwa timu ya KILIMAJARO STARS kucheza na RWANDA saa kumi jioni , UGANDA itacheza na ETHIOPIA wakati siku ya jumanne BURUNDI itacheza na ZANZIBAR na KENYA itacheza na MALAWI.
Matokeo hayo yanaifanya Bara itimize pointi sita baada ya kucheza mechi tatu huku wakishinda mbili na kufungwa moja tu.
Stars, inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager leo ilionyesha kandanda safi na kusisimua mashabiki wa Tanzania waliokuja kuiunga mkono hapa, akiwemo Mbunge wa Kondoa Kaskazini, Alhaj Juma Nkamia.
Iliwachukua sekunde 48 tu Stars kupata bao la kwanza, kupitia kwa mshambuliaji wa Simba SC, inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premum Lager pia, Mrisho Khlfan Ngassa aliyewazidi ujanja mabeki wa Somalia.

VIKOSI
Kikosi cha Stars kilikuwa; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Issa Rashid, Shomari Kapombe, Kevin Yondan, Shaaban Nditi, Mrisho Ngassa, Salum Abubakar, John Bocco, Frank Domayo na Amri Kiemba.
Somalia; Mohalim Abdullahi/Hussein Abdallah dk30, Ali Mohamed, Said Mahamud, Ali Dadir, Sadaq Abdikadir, Mohamed Salah, Abdikarim Abubakar, Abdallah Mohamed/Hamza Mukhtar, Ahmed Abdikadir Dahir/Muhad Hajji na Ali Ahmed Ali.

No comments:
Post a Comment