BUKOBA SPORTS

Monday, December 3, 2012

CECAFA TUSKER CUP 2012: KILIMANJARO STARS NA ZANZIBAR HEROES ZAPETA, WATINGA NUSU FAINALI NI BAADA YA STARS KUIFUNGA RWANDA GOLI 2-0 KWENYE UWANJA WA LUGOGO NA ZANZIBAR HEROES KUINYUKA BURUNDI KWA MISHUTI YA PENATI.

Zanzibar Heroes, mabingwa wa mwaka 1995 ambao katika mchezo wa robo fainali ya pili wamefanikiwa kuwafunga Burundi 
(Intamba Murugamba) kwa penati 6-5 baada ya dakika 90 za mchezo huo kumalizika bila kufungana. Abdallah Othman alifunga penati ya ushindi kwa Zanzibar baada ya Fiston Abdoul wa Burundi kupoteza penati yakeKIKOSI CHA ZANZIBAR HEROES KILICHOIMAILIZA BURUNDI LEONahodha wa Burundi Selemani Ndikumana na nahodha Zanzibar Nadir ‘Cannavaro’ Haroub walokosa penati zao.

Ndani ya dakika 90 mshambuliaji wa Zanzibar Juma Jaku Juma alipoteza nafasi nyingi za kumalizia huku mlinda mlango Ally Mwadini akiokoa mipira mingi iliyo elekezwa langoni kwake na Selemani Ndikumana na Christopher Nduwagira.
Wachezaji wa Zanzibar wakiwa wamembeba kipa wao, Mwadini Ally baada ya kupangua mkwaju mmoja wa penalti, na kuiwezesha timu hiyo kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge baada ya kuifunga Burundi kwa penalti 5-4 kwenye Uwanja wa Lugogo, mjini Kampala, Uganda jioni hii. Zanzibar sasa itacheza na mshindi kati ya Kenya na Malawi.(picha na BinZubeiry blog)
Penati za Zanzibar zilifungwa na Khamis Mcha Khamis, Adeyom Saleh Ahmed, Juma Jaku Juma, Nuhu Haji Samih, Aggrey Morris na Abdallah Othman wakati ambapo kwa upande wa Burundi penati zao zilifungwa na Styve Nzigamasabo, Amisi Tabwe, Christopher Nduwagira, Leopold Nkurikiye na Gael Duhatindayishimiye.

LEO, huko Kampala, Uganda, Timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, imecheza Mechi yake ya Robo Fainali ya CECAFA Tusker CHALENJI Cup dhidi ya Rwanda na kuweza kuwafunga goli 2-0 goli la kwanza limefungwa dakika ya 33 kipindi cha kwanza kupitia kwa Amri Kiemba kwa kumchambua kipa, na kilimanjaro wakapata goli la pili kipindi cha pili lililotupiwa na John Bocco.Mashabiki wa Kilimanjaro Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, wakishangilia wakati wa mchezo wa Robo Fainali ya kwanza ya michunao ya Cecafa Challenge dhidi Rwanda uliochezwa katika Uwanja wa KCC uliopo Lugogo nchini Uganda.

Shughuli imemalizika jijini Kampala, Stars imetinga nusu fainali baada ya kuichapa Amavubi mabao mawili kwa bila. Shujaa wa leo ni Mwinyi Kazimoto alietengeneza pande la maana kipindi cha kwanza katika dakika ya 33 na Amri Kiemba kumalizia Dakika ya 54 ilikuwa ni Mwinyi Kazimoto aliepiga shuti kali lililomshinda kipa wa Rwanda na John Bocco "Adebayor" akauwahi mpira na kuutupia wavuni.
 Hongera Stars!


RATIBA/ MATOKEO
ROBO FAINALI:
Jumatatu Desemba 3
[Mechi kuchezwa Lugogo Stadium]
Rwanda 0 v 2 Kilimanjaro Stars [SAA 8 MCHANA]
Burundi 5 v 6 Zanzibar [SAA 10 JIONI](Magoli ya mikwaju ya penati)

Jumanne Desemba 4
[Mechi kuchezwa Namboole Stadium]
Kenya v Malawi [SAA 10 JIONI]
Uganda v Ethiopia [SAA 1 Usiku]

No comments:

Post a Comment