FERGUSON AMTAKA MOURINHO KUVAA VIATU VYAKE OLD TRAFORD.
MENEJA wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson ameonyesha imani yake kuwa Jose Mourinho ndio meneja anayefaa kuchukua nafasi yake wakati atakapoondoka Old Traford. Ferguson mwenye umri wa miaka 70 amekuwa kocha wa United toka mwaka 1986 na bado hajaamua rasmi lini ataachia nafasi hiyo kwa ajili ya kustaafu lakini alimsifia Mourinho ambaye anaifundisha Real Madrid kuwa kocha mwenye viwango vya kuingoza United katika siku za mbeleni.
Kocha huyo amesema kuwa hakutegemea mtu ambaye hajawahi kucheza soka kama anaweza kuwa kocha bora lakini Mourinho mwenye umri wa miaka 39 amebadilisha dhana hiyo na anaweza kufundisha popote na kwa kiwango cha juu kabisa. Ferguson anakumbuka wakati Mourinho anaingia Uingereza na kujiita yeye wa kipekee na kuwaambia wachezaji wa Chelsea watashinda taji la Ligi Kuu nchini humo alimuona kama mwehu lakini alipoanza kazi alithibitisha usemi wake.
Jose Mourinho
ANDERSON NJE WIKI KADHAA!!
Sir Alex Ferguson amethibitisha Anderson atakuwa nje ya Uwanja kwa Wiki kadhaa baada ya kuumia kwenye Mechi ya Ligi Kuu England walipoifunga Reading Bao 4-3 juzi Jumamosi.
Anderson, ambaye amecheza Mechi 8 za mwisho za Man United, Jumamosi wakicheza na Reading alifunga Bao la kwanza zuri lakini ikabidi atolewe kabla haftaimu baada ya kuumia musuli za pajani.
UHALIFU HUPUNGUA PINDI CHICHARITO ANAPOKUWA AKICHEZA - POLISI.
NYOTA wa kimataifa wa Mexico na klabu ya Manchester United, Juvier Hernandez amekuwa maarufu nchini kwake mpaka kufikia hatua ya matukio ya uhalifu kupungua pindi anapocheza. Mbali na uhalifu kupungua lakini wanawake wajawazito wanaokaribia kujifungua nao hushikwa na uchungu kwa furaha pindi nyota huyo anapoifungia bao timu yake ya United hivyo idadi ya watoto kuzaliwa kuongezeka. Ofisa wa juu wa polisi wa mji mkuu wa nchi hiyo Mexico City, Jorge Carlos Martinez amesema kuwa uhalifu kama wa kuteka magari, uvamizi na ukabaji hupungua na inavyoonekana wahalifu hutumia muda huo kumuona shujaa wao wakati anacheza. Ofisa huyo wa polisi amesema kuwa ana matumaini meneja wa United Sir Alex Ferguson ataendelea kumtumia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 wakati wa kipindi hiki ambacho mji huo unakumbwa na matukio mengi ya uhalifu. Watu zaidi ya 15,000 huuliwa kila mwaka na magenge ya wauza madawa ya kulevya.
CHICHARITO akishangilia baada ya kufunga goli.
No comments:
Post a Comment