BUKOBA SPORTS

Sunday, December 9, 2012

TAMASHA LA SHANGWE LAFANA MJINI BUKOBA


Mwimbaji wa Nyimbo za Injili,Rose Muhando akitumbuiza kwenye Tamasha la shangwe Kagera katika uwanja wa Kaibata mjini Bukoba mwishoni mwa wiki,tamasha hilo lililoandaliwa na Kampuni ya Beula Communication kwa ajili ya kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika mkoa wa kagera.

Mwimbaji wa Nyimbo za Injili,Enock Jonas(Zunguka) akitumbuiza kwenye Tamasha la shangwe Kagera katika uwanja wa Kaibata mjini Bukoba mwishoni mwa wiki,tamasha hilo lililoandaliwa na Kampuni ya Beula Communication kwa ajili ya kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika mkoa wa kagera.

Masista wa Kituo cha Tumaini Children’s Centre, Sr.Adventina Kyamanywa (kushoto) na Sr.Esther wakijadiliana jambo wakati wa tamasha la shangwe Kagera katika viwanja vya Kaitaba mjini Bukoba.


Mkurugenzi wa Beula Communication, Melkzedek Mutayabarwa akizungumza kwenye Tamasha laShangwe Kagera,ambapo kampuni hiyo ndio iliyoandaa tamasha hilo.

Mkuu wa Wilaya Bukoba,Zippora Pangani akihutubia kwenye Tamasha la shangwe Kagera katika uwanja wa Kaibata mjini Bukoba mwishoni mwa wiki,tamasha hilo lililoandaliwa na Kampuni ya Beula Communication kwa ajili ya kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika mkoa wa kagera.

Waimbaji wa kwaya ya Vijana ya KKKT Usharika wa kanisa Kuu la Mjini Bukoba wakitumbuiza kwenya tamasha la Shangwe Kagera.

Rose Muhando akiwaburudisha viongozi walioudhuria Tamasha la Shangwe Kagera katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
 ___________________________________






MAKUNDI NA RATIBA YA UHAI CUP AMBAYO YATAANZA KUTIMUA VUMBI DESEMBA 11 MWAKA HUU 2012SHIRIKISHO la soka nchini leo limetoa ratiba na makundi ya timu zitakazo shiriki mashindano ya Uhai yanayodhaminiwa na Bharessa Group of Company kupitia bidhaa yake ya maji ya uhai.

Draw hiyo imechezeshwa  jana kwenye ofisi za TFF mbele ya waandishi wa habari na wawakilishi wa vilabu na ilisimamiwa na Salum Madadi ambaye ni Afisa maendeleo ya Soka wa shirikisho la Soka nchini.


Mashindano haya yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba 11 mwaka huu, jijini Dar es salaam na yatashirikisha timu 14 ambazo zimegawanywa kwenye makundi matatu kwenye viwanja vya Azam Complex Chamazi na Karume.


Kundi A na Kundi B litakuwa na timu tano tano ambapo yatatoa timu tatu zitakazoingia robo fainali na kundi C litatoa timu 2 zitakazoingia robo fainali.


Jumla ya timu 8 zitaingia robo fainali ambayo itachezwa tarehe 18 na 19 Desemba, nusu fainali itachezwa Desemba 21 na fainali ni Desemba 23.


KUNDI A 

Coastal Union
Tanzania Prison
JKT Ruvu
Mtibwa Sugar
Toto African

KUNDI B

African Lyon
Polisi Moro
Azam FC
JKT Mgambo
Simba SC

KUNDI C

Kagera Sugar
JKT Oljoro
Yanga
Ruvu Shooting


RATIBA YA KUNDI A                     RATIBA KUNDI B                   RATIBA KUNDI  C
Coastal Union vs Tanzania Prison           African Lyon vs Polisi Moro         Kagera Sugar vs JKT Oljoro
JKT Ruvu  vs Mtibwa                           Azam vs JKT Mgambo                Yanga SC vs Ruvu Shooting
Toto African vs Coastal Union               Simba SC vs African Lyon           JKT Oljoro vs Yanga SC
JKT Ruvu vs Tanzania Prison                Azam vs Polisi Moro                    Ruvu Shooting vs Kagera Sugar
Mtibwa Sugar vs Toto African               JKT Mgambo vs Simba SC         Kagera Sugar vs Yanga SC
Coastal Union vs JKT Ruvu                  African Lyon vs Azam                  JKT Mgambo vs Ruvu Shooting
Tanzania Prison vs Mtibwa                    Polisi Moro vs JKT Mgambo
Toto African vs JKT Ruvu                     Simba vs Azam
Mtibwa Sugar vs Coastal Union             JKT Mgambo vs African Lyon
Tanzania Prison vs Toto African              Polisi Moro vs Simba



Mwandishi wa Habai akiokota karatasi zenye jina la timu na kingine chenye kundi kwenye visanduku vilivyowekwa mezani tayari kwa upangaji wa makundi

No comments:

Post a Comment