BUKOBA SPORTS

Tuesday, January 1, 2013

KOCHA MPYA SIMBA ASAINI MKATABA WAKE WA MIEZI 18 WA KUINOA TIMU HIYO.


KOCHA mpya wa Simba, Patric Lieweg kutoka Ufaransa, amesaini mkataba wa miezi 18 kuitumikia klabu hiyo na kusema yeye ni mtu wa vitendo na hana muda wa kujinadi bali mashabiki wa Msimbazi wasubiri matokeo ya kazi yake.

Lieweg aliyewasili nchini jana saa 7 mchana, alisema yeye ni kocha mwenye vigezo vyote vya kuweza kuiletea mafanikio Simba, lakini hayo yote yanapaswa kuonekana uwanjani na si kwa majigambo.

“Nimekuja hapa kufanya kazi na kuhakikisha Simba inafanya vizuri katika michuano yote, lakini hakuna miujiza katika kufikia matarajio, njia pekee ni ushirikiano.

“Nahitaji muda mchache wa kukaa na timu kabla ya kuibadilisha na kupata matokeo mazuri” alisema Lieweg ambaye alipokewa na mamia ya mashabiki wa Simba. 


No comments:

Post a Comment