BUKOBA SPORTS

Sunday, February 3, 2013

AFCON 2013: SOUTH AFRICA 1 vs MALI 1, WENYEJI AFRICA KUSINI TATEMBEZEWA KICHAPO KWENYE MIKWAJU YA PENATI, WAONDOLEWA 3-1, MALI WASONGA!!

Afrika Kusini imebanduliwa nje ya mashindano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika, baada ya kulazwa magoli matatu kwa moja kupitia mikwaju ya Penalti na Mali.
Timu hizo mbili zilitoshana nguvu ya kufungana bao moja kwa moja katika dakika tisini za kawaida na hata baada ya dakika zaidi thelathini kuongezwa hakuna aliyefanikiwa kuona lango la mwenziye na hivyo mechi hiyo kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti.
Kinyume na matarajio ya wengi, wenyeji wa fainali hizo Afrika Kusini ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupiga mikwaju yake na kufanikiwa kupata mkwaju wa kwanza pekee.
Mali ilijibu kwa kufunga mikwaju mitatu na katika mkwaju wa kuamua ikiwa wataendelea, mkwaju uliopigwa na mchezaji wa Afrika kusini ulipaa juu ya goli na hivyo kuwapa Mali ushindi bila kupiga mkwaju zaidi.
Mali na Ghana tayari zimefuzu kwa nusu fainali ya mashindano hayo.
Washindi wengine wawili kuamuliwa katika mechi baina ya Nigeria na Ivory Coast na Togo na Burkina Faso leo Jumapili.
Goli la Afrika Kusini limefungwa katika dakika ya 31 na Tokelo Rantie.
Afrika Kusini ilifuzu kucheza robo fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ikiwa mshindi wa kwanza kutoka kundi A, huku Mali wakitokea kundi B wakiwa washindi wa pili.


Wachezaji wa timu ya taifa ya Mali wakishangilia baada ya kufanikiwa kuifunga Afrika kusini kwa njia ya penati katika mchezo wa pili wa robo fainali ya michuano ya mataifa ya Afrika.

Mlinda mlango wa Mali Soumaila Diakite aliibuka shujaa usiku wa jana baada ya kufanikiwa kudaka penati mbili ambazo zilipelekea matokeo ya ushindi wa penati 3-1 dhidi ya waandaji wa fainali za mataifa ya Afrika Afrika kusini na kuivusha Mali mpaka katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment