BUKOBA SPORTS

Sunday, March 17, 2013

TETESI: ARSENAL YAMUWEKA JOVETIC KATIKA RADA ZAKE.

KLABU ya Arsenal imepanga kumsajili Stevan Jovetic katika kipindi cha usajili majira ya kiangazi huku klabu hiyo ikipanga kuvunja rekodi yake ya usajili kwa mshambuliaji huyo wa Fiotentina ya Italia. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Montenegro amekuwa akifuatiliwa na meneja wa Arsenal,Arsene Wenger kwa kipindi cha miezi 18 ambapo nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 aliwekewa watu waliokuwa wakimfuatilia. Baada ya muda huo kupita Wenger ameonyesha nia ya kumuweka nyota huyo katika mipango yake ya usajili kwa kutaka taarifa kutoka kwa watu waliowekwa kufuatilia kiwango cha mshambuliaji huyo nchini Italia. Wenger anajua Jovetic hawezi kuachiwa bei rahisi na Fiorentina wamepanga kumpiga bei nyota huyo kwa kiwango kisichopungua paundi milioni 20 ambacho kitazidi rekodi ya usajili ya klabu hiyo ya paundi milioni 15 ilizotoa kwa klabu ya Zenit Saint Petersburg kwa ajili ya kumsajili Andrey Arshavin.Solution: Arsene Wenger wants Stevan Jovetic to spearhead his side next season
Solution: Arsene Wenger wants Stevan Jovetic to spearhead his side next season
History: Olivier Giroud (centre) was one of a few players Wenger got his scouts to concentrate on
History: Olivier Giroud (centre) was one of a few players Wenger got his scouts to concentrate on
Big plans: Arsene Wenger has £70m to spend in the summer
Arsene Wenger has £70m to spend in the summer


Jovetic: Vital statistics

Partizan (06-08) 13 goals in 51 apps
Fiorentina (08-13) 34 goals in 108 apps
Montenegro (07-13) 10 goals in 21 apps

No comments:

Post a Comment