BUKOBA SPORTS

Monday, June 10, 2013

KIRAFIKI: BRAZIL YAIBAMIZA FRANCE 3-0! NI USHINDI WA KWANZA WA BRAZIL KWA FRANCE TANGU 1992!

Brazil wakicheza kwao huko Gremio Arena, Porto Alegre, Usiku huu wameibamiza France Bao 3-0 katika Mechi ya Kirafiki ikiwa ni matayarisho yao kwa ajili ya ushiriki wao kama Wenyeji wa Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara yatakayoanza Juni 15.
Hadi Mapumziko Bao zilikuwa 0-0.
Kipind cha Pili, Brazil katika Dakika ya 54 kupitia Mchezaji wa Chelsea Oscar na kupiga Bao la pili katika Dakika ya 84 baada ya kaunta ataki safi ambayo ilimkuta Neymar aliempoozea Hernanes, alieingzwa Kipindi cha Pili, ambae alimalizia kifundi.

Bao la 3 la Brazil lilifungwa na Lucas Moura katika Dakika ya 93 kwa Penati baada ya Marcelo, ambae aling’ara sana Mechi hii, kuchezewa faulo na Debuchy.

Ushindi huu ni wa kwanza kwa Brazil kuifunga France katika Miaka 11 na ni kipigo cha tatu mfululizo kwa France na sasa kinaleta presha kubwa kwa Kocha wa France Didier Deschamps.
Mchezaji wa France Adil Rami kwenye patashika na mchezaji Neymar kuutwaa mpiraWachezaji wa Brazil wakifurahia ushindi baada ya kuizaba 3-0 timu ya France

No comments:

Post a Comment