BUKOBA SPORTS

Sunday, June 9, 2013

MGODI WA GEITA WAJIANDAA NA KILIMANJARO CHALLENGE 2013

Mgodi wa Geita umejiandaa na mwaka mwingine wa Kilimanjaro Challenge katika Hotel ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, Tanzania Ijumaa iliyopita. Pia ufunguzi wa hafla huo ulihusisha kutaja majina ya asasi zitakazo faidika na fedha zilizokusanywa katika upandaji mlima mnamo mwaka wa 2012.
Mpango huu kwa mara ya kwanza ulianzishwa mnamo mwaka 2002 ukihusisha wapandaji mlima 47 uliowezesha kukusanya kiasi cha fedha za kitanzania milioni 62. Ni mafanikio hayo yaliyoipa nguvu na moyo Geita Gold Mine kufanya tukio hilo la upandaji mlima kama tukio la kitaifa la kila mwaka.

No comments:

Post a Comment