Timu ya Kahororo imefanikiwa kuifunga timu ya hamugembe bao 2-1, katika michuano ya Kombe la Kagasheki Cup inayofanyika mjini Bukoba Kagera kwenye uwanja wa Kaitaba. Kahororo iliyopo kundi B wakitoka nyuma ya bao 1-0 walifunga bao la kusawazisha kipindi cha pili na bao la ushindi likafungwa dakika za mwishoni za mchezo huo.
Timu hiyo ya Kahororo iliyofungwa juzi bao mbili na timu ya Nyanga leo hii imefanya kweli nakuongeza bidii uwanjani baada ya kubadilisha baadhi ya wachezaji wake kipindi cha pili imeweza kujitetea vilivyo na kujituma. Sasa Kahororo itacheza na bakoba saa 8:00 mchana siku ya Ijumaa tarehe 19

Wachezaji wa Kahororo washangilia baada ya kusawazisha bao na kufanya 1-1 dhidi ya timu ya Hamugembe

Mashabiki wakiwapongeza wachezaji wa kahororo

Jukwaa lilikuwa halitoshi!! nyomi kutoka pande ya Kahororo na kashai walijumuika kupongeza timu ya Kahororo.

Mashabiki wakapandisha mizuka na kuingia uwanjani baada ya kufunga bao la 2

Furaha ikawa furaha!!

Wachezaji wa Kahororo pamoja na wachezaji wao wa akiba wakachanganyikana kupongezana!!!

Ushindi wa bao 2-1 ukawainua mashabiki kwenye viti!!

Wachezaji wa Kahororo wakipongezana baada ya kufunga bao la ushindi

Mzee mmoja nae akajichanganya kwa wachezaji wa Kahororo bila kujua kuwa anavunja kanuni!!angalia wakicheza hapa Ngwasuma!!! kama Wakongo!!

Jukwaani sasa!!!

Kushoto ni Rashid Kikoti mchezaji aliyefunga bao la ushindi la 2 na kufanya 2-1 dhidi ya timu ya Hamugembe wazee wa pikipiki

Nyie!!! Wachezaji wakijigamba mbele ya Kocha wao Cletus Mutakyawa (kushoto) baada ya mpira kuisha jioni hii na kuacha mtanange wa Kashai na Kitendaguro(Makhirikhiri) ukitaka kuanza.

No comments:
Post a Comment