BUKOBA SPORTS

Saturday, July 13, 2013

KIRAFIKI: SINGHA ALL STARS XI 1 vs MANCHESTER UNITED 0, DAVID MOYES AANZA NA KICHAPO KAMA MZEE FERG!!!

MABINGWA wa England, Manchester United, leo wameanza Ziara yao ya huko Barani Asia na pia Mechi ya kwanza chini ya Meneja mpya David Moyes kwa balaa baada ya kufungwa Bao 1-0 huko Bangkok, Thailand na Kombaini ya Singha All Star.
Bao la ushindi kwa Singha All Star XI lilifungwa na Teeratep Winothai Dakika za mwanzo tu za Kipindi cha Pili.
Ingawa Man United walitawala Mechi kwa muda mrefu, umaliziaji mbovu, hasa wa Danny Welbeck, ndio uliowakosesha ushindi.
Vijana Chipukizi, Adnan Januzaj na Wifried Zaha, waling’ara sana na kukosa Bao kadhaa likiwemo shuti safi la Zaha lililompita Kipa na kugonga Posti. 

Leo Usiku Man United wanasafiri kwenda Australia ambako Julai 20 watacheza na A-League All Stars ndani ya ANZ, Stadium, Mjini Sydney.
Aerial duel: Rafa da Silva fights for the ball with Nattaporn Phanrit
Rafael  da Silva akichuana na Nattaporn Phanritleo hii
Ben Amos akiondoa mpira huku  Rio Ferdinand akiruka juu mbele yake pamoja na kipa!Strike: Tom Cleverley hits the ball after getting clear of Mario Djurovski
Tom Cleverley akiachia shuti kali baada ya kumtoka Mario Djurovski
Midfield battle: Anderson takes on Thitipan Puangchan
Anderson akichuana na Thitipan Puangchan 
VIKOSI: 
Man Utd: Amos; Fabio (Evra 78), Ferdinand, Evans, Buttner (Rafael 33); Cleverley (Jones 62), Carrick, Anderson (Zaha 62) ; Januzaj, Giggs (Lingard 62); Welbeck.
 
RATIBA 
- Julai 13 Singha All Star XI (Rajamangala Stadium, Bangkok - Singha 80th Anniversary Cup) 1-0
- Julai 20 A-League All Stars (ANZ, Stadium, Sydney) SAA 6 NA  NUSU MCHANA
- Julai 23 Yokohama F-Marinos (Nissan Stadium, Yokohama) SAA 7 MCHANA
- Julai 26 Cerezo Osaka (Osaka Nagai Stadium, Osaka) SAA 7 MCHANA
- Julai 29 Kitchee (Hong Kong Stadium, Hong Kong) SAA 9 MCHANA
- Agosti 6 AIK Fotboll (Friends Arena, Stockholm) KUJULISHWA
- Agosti 9 Sevilla (Old Trafford - Rio Ferdinand Testimonial) SAA 3 NA NUSU USIKU
 

No comments:

Post a Comment