MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Uganda, Hamisi Friday Kiiza ‘Diego wa Kampala’
ametua Alasiri ya leo Dar es Salaam na ndege ya KQ tayari kusaini Mkataba
wa kuendelea kuitumikia Yanga SC kwa miaka mingine miwili.
Hiyo inafuatia mpachika mabao huyo kufikia makubaliano na Yanga juu ya dau
la usajili, baada ya awali kushindana hadi akarejea kwao, Kampala na
ikaripotiwa alikuwa karibuni kusaini URA ya kwao.
Mfanyabiashara mwenye jina mjini, Mussa Katabaro alikwea pipa hadi Uganda
wiki mbili zilizopita kufanya mazungumzo ya kina na Kiiza ili abaki Yanga
Kutoka kulia Kiiza,Katibu was Yanga, Lawrence Mwalusako, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Abdallah Bin Kleb na Seif Magari
Kiiza akifurahia baada ya Uganda kuifunga Tanzania 1-0
WWW.BUKOBASPORTS.COM

Kigogo wa usajili wa Yanga SC, Seif Ahmad 'Magari' akiwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Hamisi Friday Kiiza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya mechi kati ya Tanzania na Uganda. Kiiza amewasili Alasiri ya leo kwa ajili ya kusaini Mkataba wa miaka miwili kuendelea kuichezea Yanga SC, baada ya mvutano wa muda mrefu na uongozi wa klabu hiyo.

Kutoka kulia Kiiza,Katibu was Yanga, Lawrence Mwalusako, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Abdallah Bin Kleb na Seif Magari

Kiiza akifurahia baada ya Uganda kuifunga Tanzania 1-0
No comments:
Post a Comment