BUKOBA SPORTS

Sunday, July 14, 2013

KWELI MAJUU HAMNAZO!!!! AL FAYED: NATAKA SANAMU YA JACKO IBAKI AU NITAKATA SHARUBU ZA KHAN!!”

 MOHAMED AL FAYED amemwambia Mnunuzi wa Klabu ya Fulham, Shahid Khan, kwamba Sanamu ya Michael Jackson itabaki hapo Craven Cottage la sivyo atamkata Sharubu zake.
Baada ya kuimiliki Fulham kwa Miaka 16, Mohamed Al Fayed Jana alimuuzia Klabu hiyo Mmarekani mwenye Asili ya Pakistan, Shahid Khan.
Mbali ya kuiinua Fulham kutoka Daraja la Tatu hadi Ligi Kuu England, Al Fayed alileta maendeleo makubwa Klabuni hapo lakini Mwaka 2011 alishangaza pale alipoizindua Sanamu ya Mwanamuziki Michael Jackson nje ya Uwanja wa Fulham, Craven Cottage.

Michael Jackson alikuwa ni rafiki wa Al Fayed na Mwaka 1999 alihudhuria mechi ya Fulham hapo Craven Cottage walipocheza na Wigan. 


Wakati wa uzinduzi wa Sanamu hiyo Mwaka 2011, wakati baadhi wakionyeshwa kushangazwa kwao, Al Fayed alibatuka: "Kwa nini
Michael Jackson statue
watu waone hili ni ajabu? Wapenzi wa Soka wamefurahia hili. Ikiwa kuna wajinga hawapendi wapotelee mbali. Sitaki wawe Washabiki, kama hawaelewi na hawaamini hili basi waende kuishabikia Chelsea!"
Baada ya kukamilisha Makubaliano ya kuiuza Fulham, Fayed, alipiga Picha na Khan huku akiwa na Sharubu za Bandia huku wote wameshikilia Jezi ya Fulham.

Tribute: Fulham owner Al Fayed unveiled the controversial statue at Craven Cottage in 2011
Fulham owner Al Fayed unveiled the controversial statue at Craven Cottage in 2011
Tunnel vision: Al Fayed believes he club he has handed the club over to a 'great guy' in Khan
Al Fayed believes he club he has handed the club over to a 'great guy' in Khan

Lakini kuhusu Sanamu ya Michael Jackson, Al Fayed amesimama kidete: “Sanamu itabaki au atakuwa kwenye matatizo makubwa-nitamkata Sharubu zake mbele ya Watu!’
Family man: After ending his ownership, Al Fayed said he wanted to spend time with his grandchildren
Family man: After ending his ownership, Al Fayed said he wanted to spend time with his grandchildren

No comments:

Post a Comment