Katika Listi hiyo, England inao Wachezaji wawili, Gareth Bale wa Tottenham na Robin Van Persie wa Manchester United.
Bale ndie Mshindi wa Tuzo mbili za PFA na ile ya Waandishi wa Soka za Mchezaji Bora wa England na Van Persie ndie alikuwa Mfungaji Bora wa Ligi Kuu England.
Tuzo ya UEFA ya Mchezaji Bora ilianzishwa rasmi na Rais wa UEFA, Michel Platini, hapo Mwaka 2011 na Washindi wake tangu wakati huo ni Lionel Messi na Andres Iniesta.
Katika Wagombea hao 10, wapo pia Messi wa Barcelona na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid, Zlatan Ibrahimovic wa Paris St Germain, Mchezaji pekee anaecheza France, na waliobakia wote wanatoka Bundesliga ambao ni Wachezaji wanne wa Mabingwa wa Ulaya, Bayern Munich, Arjen Robben, Franck Ribery, Thomas Muller na Bastian Schweinsteiger huku Borussia Dortmund ikimtoa Straika wao Robert Lewandowski.
Listi hii ya Wachezaji 10 itapunguzwa na kuwa Wagombea watatu Mwezi ujao na Mshindi atapigiwa Kura na Waandishi wa Habari kutoka Nchi Wanachama wa UEFA hapo Agosti 29, Siku ambayo UEFA itaendesha Droo ya kupanga Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa Msimu wa 2013/14 huko Nyon, Uswisi.
LISTI WAGOMBEA 10:
Gareth Bale [Tottenham]
Robin van Persie [Manchester United]
Zlatan Ibrahimovic [Paris St Germain]
Lionel Messi [Barcelona]
Cristiano Ronaldo [Real Madrid]
Robert Lewandowski [Borussia Dortmund]
Arjen Robben [Bayern Munich]
Franck Ribery [Bayern Munich]
Thomas Muller [Bayern Munich]
Bastian Schweinsteiger [Bayern Munich]
No comments:
Post a Comment