BUKOBA SPORTS

Saturday, July 20, 2013

ZIARA ASIA: INDONESIA XI 0 vs LIVERPOOL 2

Majogoo Liverpool, leo wameanza Ziara yao huko Bara la Asia kwa kushinda Bao 2-0 dhidi ya Indonesia XI, Timu ambayo majuzi ilinyukwa 7-0 na Arsenal.
Mechi hiyo ilichezwa Gelora Bung Karno National Stadium, Jakarta, Nchini Indonesia na Liverpool kupiga Bao kila Kipindi.
Bao la kwanza lilifungwa katika Dakika ya 10 na Coutinho na Raheem Sterling akafunga Bao la pili katika Dakika ya 87.
Liverpool itasafiri kwenda huko Melbourne, Australia na Jumatano Julai 24 itacheza na Klabu ya Melbourne Victory.
On show: New boy Iago Aspas played 65 minutes
Mchezaji mpya Iago Aspas akicheza hapa kwa muda wa dakika 65

Taking it easy: Brendan Rodgers watches proceedings from the dugout
Kocha Brendan Rodgers akiangalia mtanange kwa makini
Getting a run out: Steven Gerrard played for the first half in sweltering heat
Steven Gerrard alicheza kipindi cha kwanza tu katika mechi hii leo

Getting stuck in: Lucas Leiva takes no chances against Taufik
Lucas Leiva kwenye patashika na mchezaji Taufik
VIKOSI:
Indonesia XI: Meiga, Maitimo, M. Roby (Sinaga 72), Igbonefo, Ruben Sanadi, Bustomi, Taufiq, Titus Bonai, Ferdinand, Boaz, Van Dijk (Boas 55).
Liverpool: Mignolet: Johnson (Kelly 65), Toure (Wisdom 65), Agger (Skrtel 65), Enrique (Robinson 46): Gerrard (Allen 45), Lucas (Henderson 65), Alberto (Assaidi 65): Downing (Ibe 65), Aspas (Borini 65), Coutinho (Sterling 65).
Subs not used: Jones, Spearing, Flanagan.
Goals: Coutinho 10, Sterling 87.


ZIARA LIVERPOOL RATIBA
Julai 13 Preston North End 0 Liverpool 4
Julai 20 Indonesia XI 0 Liverpool 2
Julai 24 Melbourne Victory (Melbourne Cricket Ground, Melbourne) SAA 7 MCHANA
Julai 28 Thailand (National Stadium, Bangkok) SAA 8 DAK 45 MCHANA
Agosti 3 Olympiacos (Anfield - Steven Gerrard testimonial) SAA 10 JIONI
Agosti 7 Valerenga (Ullevall Stadium) SAA 2 USIKU
Agosti 10 Celtic (Aviva Stadium, Dublin) SAA 1 USIKU

No comments:

Post a Comment