BUKOBA SPORTS

Saturday, July 20, 2013

COSAFA CUP: ZAMBIA WATWAA UBINGWA! SOUTH AFRICA MSHINDI WA TATU.

WAKICHEZA huko Ndola kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa, Wenyeji Zambia leo wamewabwaga Mabingwa Watetezi Zimbabwe kwa Bao 2-0 katika Fainali na kutwaa COSAFA CUP.
Awali, kwenye Uwanja huo huo, South Africa iliifunga Lesotho Bao 2-1 na kutwaa Nafasi ya Tatu.


Bao za Zambia zilifungwa na Alex N'gonga katika Dakika ya 4 kwa Frikiki murua na Bao la pili kufungwa na Mchezaji alietokea Benchi, Kabaso Chongo, katika Dakika ya 90.

No comments:

Post a Comment