
Wachezaji wa Chelsea wakipata menu.

David Luiz akifanya mazoezi mepesi huenda akacheza Jumamosi kwa sasa ni majeruhi anasumbuliwa na hamstring.
Timu ya Chelsea FC ya Uingereza ambao wapo Marekani kwa michuano iliyoandaliwa na Guinness, Jumamosi Aug 10, 2013 itashuka dimbani kupambana na AS Roma ya Italia kwenye uwanja wa RFK uliopo Washington, DC na utaanza saa 2 usiku (8:00 pm ET).
Timu ya Chelsea ambayo imepiga kambi DC na kujifua kwenye viwanja vya Catholic University leo Jumatano usiku muda si mrefu itajitupa uwanjani kupambana na timu ya Real Madrid katika mchezo wa fainali ya mashindano hayo ya Guinness Cup mpambano utakaochezewa Miami jimbo la Florida.
Mchezo wa Jumamosi ndio utahitimisha ziara ya wanadarajani nchini Marekani.
No comments:
Post a Comment