BUKOBA SPORTS

Thursday, August 8, 2013

KAJALA AJIVUNIA KUWA NA BINTI MKUBWA KWANI WANAONGEA KAMA MARAFIKI

Kajala na mwanaye Paula Paul.
Staa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja na mwanaye Paula Paul wamekuwa kama mtu na mdogo wake kutokana na kulingana vimo na kufuatana kila kona kiasi cha kuzua maswali kwa watu.
Hivi karibuni wawili hao waliambatana kwenye mwaliko wa futari iliyoandaliwa na msanii wa filamu, Aunt Ezekiel na kuwafanya mastaa wengine kudhani ni mtu na mdogo wake.
“Ni vigumu kuamini kama huyu ni mwanao, miye nilipomuana nilidhani umekuja na mdogo wako, kweli kuzaa mapema ni mali,” alisema msanii Devota Mbaga kwa niaba ya wengine waliokuwa wakishangaa.

Paula Paul.

“Huyu ni mwanangu jamani nani hajawahi kumsikia? Wengi wanadhani ni mdogo wangu, najivunia kuwa na binti mkubwa kama huyu kwani naweza kuongea naye kama rafiki yangu,” alisema Kajala.

No comments:

Post a Comment