[ DIWANI ATHUMANI - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
MNAMO TAREHE 07.08.2013 MAJIRA YA SAA 17:00 HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA NDAGA WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. PIKIPIKI T.101 CDR AINA YA T-BETTER IKIENDESHWA NA RASHID S/O ISSA, MIAKA 32, MKINGA, MKULIMA MKAZI WA KIJIJI CHA NTOKELA ILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MTOTO WILLY S/O EDWARD,MIAKA 5,MSAFWA MKAZI WA KIJIJI CHA NDAGA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA RUNGWE. CHANZO NI MWENDO KASI, DEREVA AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA KYELA - AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA
KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 07.08.2013 MAJIRA YA SAA 08:30 HRS HUKO KATIKA ENEO LA KALUMBULU WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. GARI T.932 BUF AINA YA T/IPSUM IKIENDESHWA NA KAIMU S/O HENDE, MIAKA 33, MBONDEI, MKULIMA MKAZI WA KYELA-KATI ILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MTOTO HAWA D/O GIBSON,MIAKA 6,MSAFWA,MWANAFUNZI DARASA LA KWANZA S/MSINGI MBUGANI MKAZI KALUMBULU NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA. CHANZO NI MWENDO KASI, DEREVA AMEKAMATWA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Signed by:
[ DIWANI ATHUMANI - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment