Aliongeza: “Yupo kwenye mikono mizuri! Ni wazi Baba yake na Familia yake inamwongoza vizuri. Kwa sasa sioni tatizo lolote! Pengine katika Miaka ijayo mtakuja kukumbuka haya mahojiano!”
Hata hivyo, Moyes amesema hamna uhakika kama Januzaj atacheza kwenye Mechi ya Jumamosi ya Ligi Kuu England Uwanjani Old Trafford dhidi ya Southampton.
Alifafanua: “Sidhani kama kuna Mtu anacheza kila Mechi ya Manchester United. Tuna Wachezaji wengi kubadili Timu kila Mechi. Adnan ana Miaka 18, unategemea atacheza kila Mechi? Je ni mzuri kiasi hicho? Jibu ni ndio!”
Meneja wa Manchester United David
Moyes akipeana jambo na Patrice Evra pamoja na Wayne Rooney leo ijumaa kujiweka sawa na mchezo wao pamoja Southampton hapo Old
Trafford kesho jumamosi saa 11 kamili mchana.
Patrice Evra na Robin van
Persie wakifurahia jambo, Kumbuka Van Persie ndiye ameshikilia na kuvunja historia ya Nchi yake Holland kwa kuvuja ya Patrick K. Hivi karibuni..!
Nani nae alionekana kufurahia mazoezi hayo na pia kumbuka tangu msimu huu uanze Nani amekuwa akijumuishwa kwenye kikosi cha kwanza.
No comments:
Post a Comment