BUKOBA SPORTS

Friday, October 18, 2013

MISS UNIVERSE TANZANIA AKABIDHIWA BENDERA LEO

Mrembo wa Miss Universe Tanzania 2013 Betty Boniface Omara amekabidhiwa bendera leo na waziri wa mali asili na utalii mheshimiwa Kagasheki. Zoezi hili limefanyika katika ukumbi wa mkutano wa wizara hiyo tayari kwa safari yake ya kwenda kwenye mashindano ya Miss Universe yatakayofanyika Moscow nchini Urusi mapema mwezi Novemba. Akimkabidhi bendera huku akimpongeza waziri Kagasheki pia amemtakia mafanikio mema huko aendako.
Betty pia aliwaahidi watanzania kuwa mbali na kurudi na ushindi lakini pia ataenda kuitangazia dunia kuacha kutumia nakshi (Mapambo) yanayotumia pembe za ndovu ili kumaliza tatizo la ujangili hapa Nchini.
Zoezi la kukabidhiwa Bendera lilifanyika na kushuhudiwa mbele ya Mkurugenzi wa Kitaifa Miss Universe Tanzania Maria Sarungi Tsehai.

No comments:

Post a Comment