
Kazi ipo saa 10 hii
Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa kombe la ligi kuu Tanzania bara wananolewa na kocha Ernest Brants raia wa Uholanzi na wanakaribishwa ugenini na Simba ambao wanaongoza ligi wakiwa kileleni na pointi 18.
Simba wanaoongozwa na kocha Abdallah Kibadeni wanawania kuibuka washindi ili waendeleze uongozi na kubakia kileleni endapo watafanikiwa kufikisha pointi 21 wakati Yanga inapania ushindi ili iweze kufikisha pointi 18.
Mashabiki wa klabu zote wamekuwa katika tambo za ushindi wa mtanange huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkali kama ilivyo ada kwa mechi zinazowakutanisha vigogo hao wa soka la Tanzania.
Katika mechi iliyopita Yanga ilikutana na Kagera Sugar na kuibuka na ushindi wa bao 2-1, wakati Simba ilikutana na Prisons na kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Mechi hiyo itaongozwa na mwamuzi Israel Nkongo wa Dar es salaam na waamuzi wasaidizi Hamis Chang'walu wa Dar es salaam na Ferdinand Chacha wa Bukoba huku mwamuzi wa akiba akiwa ni Oden Mbaga.
No comments:
Post a Comment